Aïda Muluneh
Aïda Muluneh (amezaliwa Addis Ababa, Ethiopia, 1974[1]) ni msanii wa kisasa na mpiga picha kutoka nchi ya Ethiopia.[2][3][4][5]
Anajishughulisha na kazi za biashara. pia ni mwandishi wa picha huko Addis Ababa.[5]
Muluneh alishinda zawadi kutoka Umoja wa Ulaya katika tuzo ya African Photography Encounters na tuzo ya CRAF International Award of Photography. Mwaka 2020, Muluneh alipewa tuzo ya utunzaji na usimamizi wa picha na jamii ya wapiga picha iitwayo Royal Photographic Society.
Wasifu
haririMaisha na malezi yake ya utotoni yalikuwa katika nchi na sehemu mbalimbali kama vile Uingereza, Yemen, Ugiriki na Cyprus kabla ya kuishi nchini Kanada mwaka 1985.[6] Kama kijana, alisoma Western Canada High School iliyopo Albert, nchini Kanada. Alikuwa katika timu ya shule ya mpira wa kikapu na alikuwa na matamanio ya kuwa nyota wa mchezo wa kikapu. Muluneh alianza kazi ya upigaji picha akiwa shuleni ila hakuitazamia ya kuwa ndiyo itakayokuwa kazi yake. Babu yake alipomtembelea na kujionea kipaji cha Muluneh, alimshauri kuendeleza kipaji chake katika Sanaa hiyo na aichukulie kama kazi na siyo fani ya mafurahisho.
Baada ya masomo yake, alifanya kazi katika shirika la Washington Post kama mwandishi wa Habari wa picha na tangu kipindi hicho, kazi zake zilionekana katika machapisho mengi.[7]
Tangu aliporudi Ethiopia amekuwa akiishi Addis Ababa.
Dhamira kuu
haririMuluneh hutumia rangi za msingi katika Sanaa yake ya upigaji picha. Rangi za mkolezo za bluu, manjano na nyekundu zilionekana kwa mbali katika michoro yake. Rangi hizo za msingi huakisi rangi za kuta za kanisa huko Ethiopia.[8]
Muluneh alisema kuwa, "kazi yake huanza na mchoro, na huifikia kila mchoro kama utengenezaji wa filamu ambapo uhusika, staili, mwanga na usanifu hutumika pamoja," alisema hayo katika usaili kwa njia ya barua pepe. "
Machapisho
haririMachapisho ya Muluneh
hariri- Ethiopia: Past, Forward. Brussels: Africalia Editions and Roularta, 2009.
- The World is 9. Johannesburg: David Krut, 2016.
Machapisho yenye michango ya Muluneh
hariri- Fiona Rogers and Max Houghton, Firecrackers: Female Photographers Now. London: Thames & Hudson, 2017.
Tuzo
haririMaonyesho
haririMaonyesho binafsi
hariri- Ethiopia Past/forward, Christiansand Kunstforening, Christianssand, [[2011]
- The World is 9, David Krut Projects, New York City, 2016
- Work from The World is Nine and 99 Series, VivaneArt, Calgary, part of Alberta’s Exposure Photography Festival, 2017[5][10]
- Reflections of Hope: Aida Muluneh in the Aga Khan Park, Aga Khan Museum, Toronto, 2018
Maonyesho ya kikundi
hariri- Ethiopian Passages - Dialogues in the Diaspora, National Museum of African Art, Smithsonian Institution, Washington, DC, 2003[9]
- Imágenes Havana, Havana, Cuba, 2003[9]
- 8th International Open, Woman Made Gallery, Chicago, IL, 2005
- Body of Evidence (Selections from the Contemporary African Art Collection), National Museum of African Art, Smithsonian Institution, Washington, DC, 2006
- Spot on..., ifa-Galerie Berlin, 2008
- Spot On… Bamako, Vii. African Photography Encounters, ifa-Galerie Stuttgart, Stuttgart, 2009
- Always Moving Forward, Gallery 44 Centre for Contemporary Photography, Toronto, ON, 2010
- The Divine Comedy - Heaven, Purgatory And Hell Revisited By Contemporary African Artists, Museum für Moderne Kunst|Museum für Moderne Kunst (MMK), Frankfurt/Main, 2014; SCAD Museum of Art, Savannah, GA
- 1:54 Contemporary African Art Fair, David Krut Projects Booth, Brooklyn, New York, 2016
- I love Africa, Festival La Gacilly-Baden Photo, Austria, 2018[4][11]
- Being: New Photography, Museum of Modern Art|MoMA, New York City, 2018
Marejeo
hariri- ↑ "Aida Muluneh (Ethiopian, born 1974)", artnet.
- ↑ 2.0 2.1 2.2 "Aïda Muluneh: founder and director Addis Foto Fest, Canada/Ethiopia". World Press Photo. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-08-30. Iliwekwa mnamo Agosti 30, 2018.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 3.0 3.1 "Ethiopia's Acclaimed Photographer Aida Muluneh Uses Visual Art to Share Her Heritage", 27 August 2018. Retrieved on 30 August 2018.
- ↑ 4.0 4.1 4.2 "Helen's Heroine - Aïda Muluneh". Retrieved on 30 August 2018. Archived from the original on 2018-08-25.
- ↑ 5.0 5.1 5.2 "Coloured skin: the body art of Aida Muluneh – in pictures", 21 February 2017. Retrieved on August 30, 2018.
- ↑ "Watch: 'Nterini' from our next cover star, Fatoumata Diawara". Songlines. Iliwekwa mnamo Agosti 30, 2018.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Moges-Gerbi, Meron. "Aida Muluneh: Changing the narrative on Ethiopia, one photo at a time", CNN Style, August 20, 2018.
- ↑ Jacewicz, Natalie (2018-04-22). "With Paint And A Camera, She's Forging A New Artistic Vision Of Africa". NPR.org. Iliwekwa mnamo 2019-11-06.
- ↑ 9.0 9.1 9.2 9.3 "'The testament to one's strength is determined on what we choose to do with the challenges that we face'", 9 December 2014. Retrieved on 30 August 2018.
- ↑ "Aida Muluneh - VivianeArt". vivianeart.gallery. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-09-04. Iliwekwa mnamo 30 Agosti 2018.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Africa, Baden and Honorary Fellows", 2018-07-06. Retrieved on 30 August 2018. Archived from the original on 2018-11-13.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Aïda Muluneh kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |