Abeti Masikini
Elisabeth Jean Finant (alitambulika sana kwa jina la kisanii kama Abeti Maskini; 9 Novemba 1954 - 28 Septemba 1994) alikuwa mwanamuziki maarufu wa dansi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Abeti Masikini | |
---|---|
Abeti Maskini mnamo 1989.
| |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Elisabeth Jean Finant |
Amezaliwa | Kisangani, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo | Novemba 9, 1954
Amekufa | Septemba 28, 1994 (umri 39) Paris, Ufaransa |
Aina ya muziki | muziki wa dansi, soukous |
Kazi yake | mwimbaji/mtunzi wa nyimbo, mwanamuziki |
Ala | Sauti |
Miaka ya kazi | 1971 - 1994 |
Studio | RCA Records, Polygram Records |
Katika Afrika Mashariki alijulikana sana kwa kuimba Kiswahili, hasa ule wimbo wake wa "Likayabo" (Manjano na amdalasini).
Abeti alikuwa chotara kama Jolie Detta, baba yake mzazi akiwa ni mchanganyiko wa Mkongomani na Mbelgiji.
Muziki na maisha
haririAbeti alikuwa fundi wa muziki akiwa katika umri mdogo sana ambao hakuna aliyetegemea hasa kwa jinsia yake. Mbali na hapo, alifanikiwa kuwawezesha wasanii waliokuja kuwa wakubwa baadaye, Mbilia Bel na Tshala Muana. Mbilia alikaa katika chungu cha Abeti na kupikwa vilivyo kuanzia kuimba hadi kunengua kuanzia mwaka 1976 hadi 1981. Tshala Muana yeye kuanzia mwaka 1978 hadi 1979. Yondo Sister alipikwa na Abeti katika mwaka 1986. Mwingine ni mwanamama Abby Surya (1984 - 1986).
Kwa upande wa wanaume ambao walifanya kazi na kuinuliwa na mwanamama huyu ni pamoja na Malage De Lugendo, Lokua Kanza na Komba Bellow. Ujuvi wa muziki wake ulipelekea wasanii wengine wa muziki wa soukous kama Aurlus Mabele kupenda kazi za Abeti kupita kiasi. Sifa yake kubwa na ambayo aliwaathiri kidogo Mbilia Bel Tshala Muana ni kupenda kutunga au kuimba nyimbo zake kwa lugha ya Kiswahili. Mfano ni wimbo wake wa Likayabu (Manjano na amdalasini), na hata albamu yake ya Kupepesuka ya mwaka 1978.
Baba yake, mzee Jean Finant aliuawa kikatili mwaka 1961 mjini Mbuji Mayi kutokana na matatizo ya kisiasa akiwa mfuasi wa Chama cha Hayati Patrice Lumumba ambapo mama yake alilazimika kuhama nao na ndipo wakahamia jijini Kinshasa ambako aliendelea na masomo hadi alipohitimu sekondari na baadaye kupata bahati ya kuajiriwa katika Ofisi ya Waziri wa Utamaduni wakati huo Waziri akiwa Mhe. Pierre Mushete. Kwa upenzi wa muziki, ilimlazimu aache kazi huko wizarani na kuendelea na muziki.
Mwaka wa 1971 yaliandaliwa mashindano ya kutafuta mwanamuziki chipukizi na yeye akamuua kujitosa. Yumkini kuwepo kwake kufanya kazi katika Ofisi ya Wizara hiyo kulimlazimu aachie ngazi ili pasionekane kuwepo tashwishi ya upendeleo endapo angetwaa taji. Akaacha kazi. Hata hivyo aliambulia kuwa mshindi wa 3 katika mashindano hayo,ambayo kimsingi ndio chimbuko rasmi la Abeti Masikini.
Abeti alizaliwa tarehe 9 Novemba 1954 mkoa wa Kisangani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kufariki tarehe 28 Septemba 1994 huko jijini Paris, Ufaransa.[1]. Alifariki kwa ugonjwa wa saratani ya titi.
Baadhi ya albamu
hariri1973: Pierre Cardin présente Abeti (Pathé Marconi)
1974: La voix du Zaire, l'idole de l'Afrique (Pathé Marconi)
1976: Abeti à Paris (Pathé Marconi)
1977: Abeti Masikini (Edition la Boétie)
1977: Visages (RCA)
1978: Abeti: Kupepe Suka (RCA)
1980: Mokomboso (Edison)
1981: Dixième anniversaire (Safari Ambiance)
1982: Abeti:I love you
1983: Abeti: Naleli (Zicka Production)
1984: Abeti/ Eyenga Moseka : le duo du siècle (Bade Star Music/IAD)
1984: Sens unique (Bade Star Music/IAD)
1985: Ba mauvais copiste (Bade Star music)
1985: Samoura (Bade Star Music )
1986: Je suis fachée (Bade Star Music)
1987: En colère (Bade Star Music)
1988: Scandale de jalousie "maxi 45 tours" (Polygram)
1990: Reine du soukouss (AMG/Polygram)
1996: Best of souvenirs souvenirs vol 1 (Declic)
1997: Best of souvenirs souvenirs vol 2 (Declic)
2005: 1ER Best of (Akuesson World Wide)
Marejeo
hariri- ↑ Abeti Masikini Finant Elisabeth 1954 -1994 Universal Rumba.
Viungo vya Nje
hariri- Abeti Masikini katika Allafrica.com