African Methodist Episcopal Church

African Methodist Episcopal Church (kifupi: A.M.E. Church, au Kanisa la Kimethodisti la Kiaskofu la Kiafrika) ni kanisa la kwanza lililoanzishwa na Wamarekani Weusi katika Marekani.

Askofu Richard Allen, mwanzilishi wa Kanisa la A.M.E.

Lilianzishwa na mchungaji Richard Allen mjini Philadelphia, Pennsylvania mnamo mwaka 1816, wakati makanisa kadhaa ya Wamethodisti Weusi walitafuta njia za kujitegemea kutoka kanisa kuu lililokuwa mikononi mwa Wakristo Weupe katika jamii yenye ubaguzi wa rangi.

Allen alibarikiwa kuwa askofu mnamo 1816 akisimamia wachungaji 8 na makanisa 5. Hadi mwaka 1846 walikuwa tayari wachungaji 176, makanisa 296 na Wakristo 17,375; waliongezeka kuwa 207,000 mnamo 1876.[1]

Leo hii kuna takriban Wakristo 2,510,000 wanaohudumiwa na wachungaji 3,817 na maaskofu 21 katika shirika 7,000 [2]zilizopangwa kwa mikoa katika Marekani, lakini pia huko Angola, Benin, Burundi, Cote d'Ivoire, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Namibia, Rwanda, Afrika Kusini, Togo, Uganda, Bahamas, Guyana, Jamaika, Trinidad na Tobago, Ufalme wa Maungano (Uingereza) na Kanada.

Kanisa la A.M.E ni sehemu ya familia ya makanisa ya Wamethodisti likifuata mafundisho ya John Wesley.

Tanbihi hariri

  1. The Annual Cyclopedia 1866, p 492
  2. African Methodist Episcopal Church kwenye tovuti ya World Council of Churches, iliangaliwa mnamo Januari 2017

Viungo vya nje hariri