Baraka ni tendo la kumtakia au kumuombea mtu mema, hasa kutoka kwa Mungu. Pengine mtendaji ana mamlaka fulani juu ya yule anayeombewa (kwa mfano ni mzazi), hasa katika dini husika (kwa mfano ni kuhani).

Picha takatifu ya Yesu Kristo Pantokrator iliyochorwa na Theofane Mgiriki (karne ya 14). Mkono wake wa kulia umeinuliwa ili kubariki.

Baraka zinaweza kulenga maisha ya kawaida (afya, uhai, uzazi, amani, mafanikio n.k.) au mema ya kiroho zaidi (utakaso).

Uyahudi

hariri
 
Isaka akimbariki Yakobo, mchoro wa Govert Flinck (Rijksmuseum Amsterdam).

Uyahudi ulistawisha sana baraka (kwa Kiebrania בּרכה, berâkhâh, wingi ni Berakhot) hasa kwa ibada za Hekalu la Yerusalemu, lakini pia nyumbani.

Mara nyingi hizo baraka zilitolewa baada ya mtu kutimiza amri fulani ya Mungu (mitzvah).

Muhimu kuliko zote ni Baraka ya kikuhani iliyotolewa na mwanamume wa ukoo wa Haruni (kohen) inavyoelekezwa katika kitabu cha Hesabu 6:23-27.

Ukristo

hariri

Kufuatana na urithi wa Uyahudi na wa Yesu mwenyewe hasa katika Kupaa mbinguni, Ukristo toka mwanzo ulitumia baraka katika liturujia yake, hasa kama hatima.

Ni hivyo katika Makanisa ya mashariki na ya magharibi vilevile.

Neno la Kigiriki lenye maana ya kubariki ni εὐλογία, eulogia, ambalo kama lile la Kilatini (benedictio) linaundwa na maneno mawili (εὐ, bene, vizuri + λογία, dictio, usemi). Neno la Kiingereza (benediction) na la lugha nyingine mbalimbali limekopwa kutoka Kilatini.

Baraka inaweza kutoka neno kwa neno katika Biblia (kwa mfano kutoka Nyaraka za Mtume Paulo), au kutungwa na mtoaji au kuwa na mchanganyiko wa hayo mawili.

Moja kati ya ibada zinazopendwa zaidi na Wakatoliki ni baraka kuu, ambayo inatolewa na mkleri kwa kushika mikononi Mwili wa Kristo baada ya kuuabudu kwa muda fulani, hata masaa, ukiwa juu ya altare umezungukwa na mishumaa.

Katika Kanisa Katoliki[1] zina pia umuhimu wa pekee baraka ya Papa au ya mwakilishi wake [2] na baraka ya mwisho kwa wagonjwa mahututi [3].

Kati ya Waorthodoksi baraka zinatumika kwa wingi zaidi, hata mwanzoni kabisa mwa ibada. Hata hivyo ya mwisho ndiyo muhimu zaidi. Padri anabariki kwa mkono wa kulia, ila askofu kwa mikono yote miwili. Baraka za fahari zaidi zinaweza kutolewa kwa kutumia sanamu ndogo ya msalaba.

Katika madhehebu mengi ya Uprotestanti, kiongozi wa ibada ananyosha mikono juu ya waumini kama alivyoelekeza Martin Luther katika Deutsche Messe.[4] [5]

Uislamu

hariri

Katika Uislamu hakuna ukuhani, lakini muumini yeyote anabariki wenzake kwa kuwaambia kila wanapokutana السلام عليكم ورحمة الله وبركاته, as-salāmu alaikum wa rahmatul-lāhi wa barakātuh, yaani "Amani, huruma na baraka za Mungu viwe juu yenu".

Tanbihi

hariri
  1. Kwa baraka zake mbalimbali kwa Kiswahili, taz. Misale ya Waamini, toleo la mwaka 2021, uk. 1439-1494
  2. Apostolic Benediction
  3. "last blessing"
  4. Precht, Fred L. Lutheran Worship History and Practice. St. Louis: Concordia Publishing House, 1993. p. 434.
  5. Karen B. Westerfield Tucker (8 Machi 2001). American Methodist Worship. Oxford University Press. uk. 9. ISBN 9780198029267. Iliwekwa mnamo 16 Februari 2015. In the 1824 Methodist Episcopal Discipline, instructions for the use of the Lord's Prayer and the apostolic benediction (2 Corinthians 13:14) were added, with the former to be used "on all occasions of public worship in concluding the first prayer," and the latter at the dismissal.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.