Agapio, Sekondino na wenzao

Agapio, Sekondino na wenzao (walifia dini Constantine, leo nchini Algeria, 259) walikuwa Wakristo waliouawa kwa ajili ya imani yao wakati wa dhuluma ya kaisari Valeriani.

Agapio na Sekondino walikuwa maaskofu, Emiliani alikuwa askari, Tertula na Antonia walikuwa mabikira. Pia aliuawa mama mmoja pamoja na watoto wake pacha[1].

Tangu kale wanaheshimiwa kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 4 Mei[2].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. https://www.santiebeati.it/dettaglio/92632
  2. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.