Constantine ni mji wa Algeria, wa tatu kwa wingi wa watu (448,000 mwaka 2008), na makao makuu ya wilaya ya Constantine.

Mji wa Constantine, Algeria
Mji wa Constantine, Algeria

Historia

hariri

Constantine, kwa jina la Cirta, ulikuwa mji mkuu wa ufalme wa Kiberber wa Numidia; mji wake muhimu uliopangiwa kimkakati kama bandari uliitwa Russicada. Ingawa Numidia ilikuwa na uhusiano muhimu na jamhuri ya Roma kipindi cha vita vya Karthago (264 - 146 KK), mji Cirta ulikuwa mhanga wa uvamizi kipindi cha karne ya 1 na 2 kabla ya Kristo. Hatimaye uliangukia chini ya utawala wa Kirumi wakati wa kaisari Julius. Cirta ulitawaliwa na Warumi katika kipindi cha Kaisari na cha Augustus na ulizungukwa na maeneo ya "shirikisho la miji huru ya Roma" kama Chullu, Rusicade, na Milevum, uliongozwa mwanzoni na Publius Sittius.

Mji uliharibiwa mwanzoni mwa karne ya 4 ukajengwa upya na kaisari wa Roma Konstantino Mkuu, ambaye aliupa mji huo jina jipya la Constantine. Wavandali waliuharibu mji wa Cirta, lakini kaisari Justinian I akaunyakua na kuurekebisha mji huo wa Waroma.

Ulipungua umuhimu wake baada ya uvamizi wa Waislamu, lakini jamii ndogo iliendelea kwa muda wa karne kadhaa. Magofu yake yamefanywa kama makumbusho ya kihistoria.

  Makala hii kuhusu maeneo ya Algeria bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Constantine kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.