Alberiko wa Citeaux

(Elekezwa kutoka Alberiko)

Alberiko wa Cîteaux, O.Cist. (pia Aubrey; alifariki Citeaux, 26 Januari 1109) alikuwa mkaapweke, mmonaki, halafu (1100) abati wa Neumünster nchini Ufaransa, akiongoza monasteri hiyo kwa juhudi zote pamoja na kulea wanajumuia kadiri ya upendo na kanuni.

Bikira Maria akimpa Alberiko kanzu ya Wasitoo.

Ni kati ya waanzilishi wa urekebisho wa Citeaux wa shirika la Benedikto wa Nursia. Ndiye aliyepata kutoka kwa Papa Paskali II hati Desiderium quod iliyoupatia urekebisho huo uhalali wake.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 26 Januari[1], pengine pamoja na wenzake Roberto wa Molesme na Stefano Harding.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

  • Attwater, Donald and John, Catherine Rachel John, 1993:The Penguin Dictionary of Saints. 3rd edition. New York: Penguin Books. ISBN|0-14-051312-4

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.