Alberto wa Yerusalemu

Alberto wa Yerusalemu (alizaliwa Castel Gualtieri, Italia, karne ya 12 - alifariki Akka, Israeli, 14 Septemba 1214) alikuwa kwanza kanoni, halafu askofu wa Bobbio, halafu wa Vercelli nchini Italia, halafu tena wa Yerusalemu katika Nchi Takatifu[1].

Sanamu yake huko Milano.

Ndiye aliyewapa kanuni watawa Wakarmeli. Aliuawa kwa upanga na mtu aliyekuwa amemlaumu na kumshusha cheo.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe ya kifo chake[2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.