Angel Bernard

Mwimbaji wa kike kutoka Tanzania.


Angel Bernard (alizaliwa tarehe 29 Juni mwaka 1989) ni mwimbaji kutoka Tanzania.[1]

Angel Bernard
Alizaliwa 29 Juni 1989
Nchi Tanzania
Kazi yake Mwanamuziki wa Injili

Maisha hariri

Angel ni mtoto wa tatu katika familia ya watoto sita. Ameanza kupenda uimbaji tangu akiwa na umri mdogo na alianza kuimba akiwa na umri wa miaka 6 katika Kanisa Katoliki la Tabata magengeni, akiwa mshirika wa kwaya kuu.[2]

Angel alisoma shule ya msingi Kisutu. Alifanikiwa kujiunga na shule ya Sekondari Zanaki ambapo alisoma Kidato cha kwanza hadi cha nne na pia aliweza kuendelea na kidato cha tano na cha sita katika shule hiyo hiyo. [3]

Kabla ya mwaka 2007 Angel alikuwa akiimba mchanganyiko wa nyimbo za dini na za kawaida; aliamua rasmi kuimba nyimbo za dini tu tarehe 26 Septemba mwaka 2007 katika kanisa la Mito ya Baraka jijini Dar es Salaam.[4]

Mwaka 2008 alirekodi albamu ya kwanza iitwayo Yote yalikwisha. Mwaka 2010 alirekodi albamu nyingine iliyoitwa Nitakuabudu milele.

Angel amekua akijihusisha na vikundi mbalimbali vya muziki kama vile Messengers band, Whispers Band, Glorious Celebration (GWT) na Pure Mission.

Pamoja na kuimba, Angel pia ni mzungumzaji katika maeneo mbalimbali, ni mshauri wa vijana, hasa wasichana, ni mwalimu wa sauti na pia mwandishi wa nyimbo.

Tarehe 21 Mei 2015 Angel alichumbiwa na Godsave Sakafu na kufunga naye ndoa mwezi Julai 2015. Sasa wanaishi pamoja Arusha.[5]

Tazama pia hariri

Viungo vya nje hariri

Marejeo hariri

  Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Angel Bernard kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.