Anselmo wa Nonantola

Anselmo wa Nonantola (Cividale del Friuli, 723 - Nonantola, 803) alikuwa mtawala wa Friuli miaka 749-751, lakini aliacha siasa akatawa katika monasteri mbili alizozianzisha akafanywa abati wa ile karibu na mji wa Nonantola, Italia, aliyoiongoza kwa miaka 50 akihamasisha nidhamu ya kimonaki kwa maisha na mafundisho yake[1].

Mt. Anselmo akianzisha monasteri ya Nonantola.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 3 Machi[2].

Tazama pia hariri

Marejeo hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.