Nzi mbuai
Nzi mbuai | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Alcimus sp. aliyekamata panzi wa jenasi Acrida nchini Afrika Kusini
| ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||
Nusufamilia 14:
|
Nzi mbuai au nzi wawindaji ni nzi wadogo hadi wakubwa wa familia Asilidae katika oda Diptera wanaowinda wadudu wengine. Kwa kawaida wana nywele nyingi kama manyoya na mdomo mkali unaotumika kwa kudunga mbuawa. Miguu ina nywele ndefu na ngumu sana ambayo inawasaidia kukamata wadudu. Nzi hawa ni mbuai wakali sana.
Maelezo
haririKwa ujumla wapevu ni wadogo kiasi hadi wakubwa na wengi wana urefu wa mwili wa mm 10-20. Hata hivyo, baadhi wanaweza kuwa wadogo kama mm 3 huku wengine wakifikia angalau mm 60, kama spishi ya Madagaska Microstylum magnum, nzi mbuai mkubwa kabisa anayejulikana, ambaye ana upana wa mabawa ya mm 84. Kwa kawaida mwili wao limerefuka mwenye fumbatio refu inayopunguka, lakini pia kuna spishi zilizoshindamana zenye fumbatio pana. Kutikulo imefunikwa kizito kwa nywele, haswa kwenye kichwa na thoraksi, ambayo inaweza kuwafanya kufanana na nyukibambi. Mara nyingi rangi ni za mwonekano kama vile kahawia, nyeusi na/au kijivu pamoja na rangi tofauti tofauti kama vile nyekundu na njano. Mara nyingi wako aposematiki na kuiga rangi za nyigu au nyuki.
Kichwa ni huru na kinaweza kusogea na kina macho makubwa yaliyojitokeza katika jinsia zote mbili ambayo huwapa uwezo wa kuona mbuawa kwa urahisi. Kuna kibonde kati ya macho, ambayo ni sifa ya nzi mbuai na ambamo oseli tatu ziko. Upande wa juu wa kichwa una safu kadhaa za nywele ngumu. Sekini nene ya nywele ngumu ipo kwenye uso inayoitwa mystax. Inasaidia kukinga kichwa dhidi ya wadudu mbuawa wanaojaribu kujihami.
Vipapasio ni kawaida ya nusuoda Brachycera vyenye pingili 3, ambazo ya tatu hubeba nywele ngumu ndefu (arista) au kiambatisho kinene zaidi chenye pingili moja au mbili (stylus). Sehemu za mdomo zina umbo la pua fupi na kali ambayo inatoholewa kwa kutoboa na kufyonza.
Thoraksi ni imara na imeshindamana na kubeba nywele ngumu ndefu (macrochaete). Miguu ni mirefu kiasi na ina nguvu yenye macrochaete nyingi ambazo husaidia kushikilia mbuawa. Mabawa yamekuzwa vizuri, mara nyingi membamba kwa kuruka kwa kasi. Mabawa mara nyingi ni mangavu, lakini wakati mwingine ya moshi au rangi nyeusi, kwa sehemu au kabisa.
Fumbatio ina pingili sita hadi nane zinazoonekana na kutangulia sehemu za uzazi kwa madume, lakini pingili ya nane pengine hufichwa kabisa au kwa kiasi na huunda oviposito kwa majike.
Lava ni wa aina ya buu. Ana umbo la mcheduara na amerefuka, bapa kwa kadiri fulani kutoka juu hadi chini na kupunguka kwenye ncha za pande za kichwa na mkia. Hana miguu. Rangi ni nyeupe au njano iliyofifia. Kichwa ni kidogo, kigumu, cheusi na sehemu za mdomo ziko upande wa chini.
Bundo ni uchi wenye miguu huru na kwa hivyo anaweza kusogea.
Spishi za Afrika ya Mashariki
hariri
|
|
Picha
hariri-
Machimus fimbriatus nchini Uturuki
-
Neolophonotus sp. nchini Afrika Kusini