Bahari ya Beaufort

Bahari ya Beaufort ni bahari ya pembeni ya Bahari Aktiki[1].

Bahari ya Beaufort; mstari mwekundu ni mpaka baina ya Alaska (Marekani) na Kanada. Pembetatu ya buluu nyeusi ni eneo linalodaiwa na nchi zote mbili.

Iko upande wa kaskazini wa pwani za Alaska (Marekani) na majimbo ya Yukon na Kaskazini-Magharibi ya Kanada.

Upande wa magharibi inakutana na Bahari ya Chukchi, upande wa mashariki inapakana na visiwa vya Aktiki vya Kanada.

Jina lake lilichaguliwa kwa heshima ya Francis Beaufort (17741857) aliyekuwa mtaalamu wa ramani za bahari katika jeshi la majini la Uingereza wakati wa karne ya 19.

Sehemu hii ya bahari ina eneo la kilomita za mraba 476,000 na kina chake inafikia hadi mita 4,683, kina cha wastani ni mnamo mita 1,000. Chini ya bahari kuna akiba za mafuta na gesi.

Bahari imefunikwa na barafu sehemu kubwa ya mwaka. Kuna nyangumi wengi aina ya Beluga. [2].

Eneo lenye umbo la pembetatu kwenye mpaka wa Marekani na Kanada linadaiwa na nchi zote mbili, umuhimu wake uko katika swali la haki ya kuamulia matumizi ya malighafi hizi.

Mto mkubwa unaopeleka maji yake baharini ni mto Mackenzie wa Kanada.

Tanbihi

hariri
  1. John Wright (30 Novemba 2001). The New York Times Almanac 2002. Psychology Press. uk. 459. ISBN 978-1-57958-348-4. Iliwekwa mnamo 29 Novemba 2010.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Beaufort Sea, Encyclopædia Britannica on-line