Bahari ya Liguria
Bahari ya Liguria ni sehemu ya Bahari Mediteranea iliyoko upande wa magharibi wa rasi ya Italia.
Umbo lake ni kama pembetatu kuanzia mpaka wa Italia na Ufaransa, hadi rasi ya kaskazini ya kisiwa cha Korsika na tena hadi rasi ya San Pietro (44°03′N 9°50′E / 44.050°N 9.833°E) karibu na mji wa La Spezia, Italia.[1]
Bahari hii inapokea maji ya mto Arno pamoja na mito mingine inayotelemka kutoka milima ya Apenini.
Bandari muhimu zaidi ni Genova, La Spezia na Livorno.
Kina kirefu cha kufikia mita 2,850 kinapatikana karibu na Korsika.
Picha
haririMarejeo
hariri- ↑ "Limits of Oceans and Seas, 3rd edition" (PDF). International Hydrographic Organization. 1953. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2011-10-08. Iliwekwa mnamo 7 Februari 2010.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Viungo vya nje
haririWikimedia Commons ina media kuhusu: