Batinilhuti
Batinilhuti ni nyota angavu kwenye kundinyota la Mara.[1] Iko kaskazini kwa Mraba wa Farasi na inaonekana kwa wangalizi walioko kaskazini kwa latitudo 54° Kus. Kwa kawaida hutumiwa na watazamaji nyota ili kufika Majarra ya Mara. Majarra Roho wa Batinilhuti (NGC 404) iko dakika saba za tao kutoka Batinilhuti.
Nyota hii ina mwangaza unaoonekana wa 2.07, ukibadilika kati ya 2.01 na 2.10. Hivyo wakati fulani nyota ni angavu kuliko zote kwenye kundinyota, ikiwa nyotabadilifu. Kwa mujibu wa vipimo vya paralaksi, iko takribani miakanuru 197 kutoka Jua. Mwangaza wake halisi unapunguzwa kwa 0.06 na gesi na vumbi kati ya Dunia na nyota hiyo . Nyota ina kasimwelekeo penyo ndogo ya 0.1 km/s, lakini ina mwendo halisi mkubwa kiasi, ikisafiri kwenye tufe ya anga kwa kasi ya 0.208"/mwaka.
Jina
haririJina la Batinilhuti lilijulikana tangu karne nyingi kati ya mabaharia Waswahili waliotumia nyota hii kama msaada wa kukuta njia yao baharini wakati wa usiku. Asili ya jina ni Kiarabu Baṭn al-Ḥūt, inayomaanisha "batini ya samaki".[2] Al-Ḥūt inatokana na jina la mojawapo ya makundinyota ya kale ya Waarabu, lakini lilikuwa tofauti na kundinyota la kisasa la Hutu (Samaki).[3]
Jina lake la Bayer ni β Andromedae.
Marejeo
hariri- ↑ Kamusi ya Kiswahili Sanifu (tol. la 4). Dar es Salaam: TUKI. 2019. uk. 40. ISBN 978 019 574616 7.
- ↑ Allen, R. A. (1899), Star-names and Their Meanings, uk. 36
- ↑ Davis, George A. (1971). Selected List of Star Names. uk. 5.
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Batinilhuti kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |