Ngarara
Ngarara | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Ngarara mamba (Tylosurus crocodilus)
| ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Jenasi 10 na spishi 35, 9 katika Afrika:
|
Ngarara, ngarengare, watumbuudau, watumbuu, mgendi, mgezi au mikule ni samaki za baharini na maji baridi wa familia Belonidae katika oda Beloniformes.
Maelezo
haririNgarara ni wembamba na huwa na urefu wa sm 3 hadi 95. Wana pezimgongo moja lililopo nyuma sana kwenye mwili, takriban mkabala na pezimkundu. Sifa yao bainifu zaidi ni domo lao refu na jembamba, ambalo huwa na meno mengi makali. Katika spishi nyingi taya la juu linafikia urefu wake kamili wakikomaa, hivyo wana wanaonekana kama chuchunge wenye taya la chini lililorefuka lakini lile la juu dogo zaidi sana. Wakati wa hatua hii ya maisha yao, hula planktoni na kubadilisha mpaka samaki baada ya kukomaa kikamilifu kwa domo. Ngarara huzaana kwa kujamiiana na kutaga mayai. Kwa kawaida dume hupanda jike juu ya mawimbi wakati wakijamiiana.
Ekolojia
haririNgarara wote hujilisha hasa kwa samaki wadogo, ambao wanawakamata kwa msogeo kasi kuelekea juu wa kichwa chao. Aidha, spishi fulani hukamata pia krili, gegereka wanaoogelea na sefalopodi wadogo. Spishi za maji ya chumvi ni mbuai pia na angalau spishi ya Uhindi hujilisha kwa gegereka wakubwa tu.
Ngarara wapo kawaida katika nusutropiki, lakini baadhi hukaa maji ya wastani pia, hasa wakati wa baridi. Ngarara wa Ulaya, spishi ya kawaida ya Bahari ya Atlantiki ya Kaskazini, huogelea mara nyingi kwa makundi pamoja na jodari. Hupatikana katika makazi ya maji kame ya bahari au karibu na uso wa bahari ya wazi. Jenasi kadhaa zinajumuiya spishi zilizopatikana katika mazingira ya maji ya bahari, maji ya chumvi kidogo na maji baridi (k.m. Strongylura), lakini jenasi chache zinatokea kwenye mito na vijito ya maji baridi (k.m. Belonion, Potamorrhaphis na Xenentodon).
Hatari kwa binadamu
haririNgarara, kama Beloniformes wote, wanaweza kufanya miruko mifupi nje ya maji kwa mbio za hadi km 60 kwa saa. Kwa sababu ngarara huogelea karibu na uso wa maji, mara nyingi huruka kupitia sitaha ya mashua madogo badala ya kuzunguka. Utenzi huu wa kuruka unaongezwa sana na mwanga wa bandia usiku. Wavuvi wa usiku na wazamaji katika maeneo ya Bahari ya Pasifiki wamekuwa "wakishambuliwa" na makundi ya ngarara waliochochewa ghafla wakiruka juu ya maji kuelekea chanzo cha mwanga kwa kasi kubwa. Madomo yao makali yanaweza kusababisha majeraha ya kutoboa mbali yakikonyoleka mara nyingi ndani ya mwathirika. Kwa jamii nyingi za jadi za Visiwa vya Pasifiki, ambazo huvua samaki juu ya miamba ya marijani kutoka kwenye mashua madogo, ngarara huwa hatari ya kuumia zaidi kuliko papa.
Spishi za Afrika
hariri- Ablennes hians, Ngarara Bapa (Flat needlefish)
- Belone belone, Ngarara wa Ulaya (Garfish)
- Petalichthys capensis, Ngarara Kusi (Cape needlefish)
- Platybelone argalus, Ngarara Mkuku (Keeltail needlefish)
- Platybelone a. annobonensis, Ngarara wa Anobon (Annobon keeltail needlefish)
- Platybelone a. platura, Ngarara Arabu (Arabian keeltail needlefish)
- Platybelone a. platyura, Ngarara Mashariki (Keeled needlefish)
- Platybelone lovii, Ngarara wa Kaboverde (Cape Verde needlefish)
- Strongylura leiura, Ngara Milia (Banded needlefish)
- Strongylura senegalensis, Ngarara Magharibi (Senegal needlefish)
- Tylosurus acus
- Tylosurus a. acus, Ngarara wa Maroko (Agujon needlefish)
- Tylosurus a. imperialis, Ngarara wa ??? (??? needlefish)
- Tylosurus a. melanotus, Ngarara Utaya-mkuku (Keel-jawed needlefish)
- Tylosurus a. rafale, Ngarara Magharibi-kusini (Southwest African needlefish)
- Tylosurus choram, Ngarara wa Bahari ya Shamu (Red Sea houndfish)
- Tylosurus crocodilus, Ngarara Mamba (Houndfish)
Picha
hariri-
Ngarara bapa
-
Ngarara wa Ulaya
-
Ngarara mkuku
-
Ngarara wa Bahari ya Shamu
Marejeo
hariri- Rashid Anam & Edoardo Mostarda (2012) Field identification guide for the living marine resources of Kenya. FAO, Rome.
- Gabriella Bianchi (1985) Field guide to the commercial marine brackish-water species of Tanzania. FAO, Rome.