Ibuti la Jauza

(Elekezwa kutoka Betelgeuse)

Ibuti la Jauza (jina la kisayansi Alpha Orionis, kwa Kiingereza Betelgeuse) ni nyota ya aina ya jitu jekundu inayoonekana katika kundinyota Jabari (Orion).

Mshale wa rangi ya pinki unaoelekeza nyota upande wa kulia yenye alama ya α unaonyesha Ibuti la Jauza (Betelgeuse) katika kundinyota ya Jabari (Orion)
Ibuti la Jauza (Betelgeuze) ni jitu jekundu; kushoto: inavyoonekana kwa darubini; kulia: Ibuti la Jauza (Betelgeuze) ni nyota angavu juu kushoto kwenye kundinyota ya Jabari (Orion) mara nyingi huonekana nyekundu kwa macho matupu.

Jina

Jina la Ibuti la Jauza lilijulikana tangu karne nyingi kati ya mabaharia Waswahili waliotumia nyota hii kama msaada wa kukuta njia yao baharini wakati wa usiku. Asili ya jina ni Kiarabu إبط الجوزاء (ibt al jauza) . Ibuti inamaanisha "kwapa" na Jauza ni ni jina la zamani kwa Jabari, kwa maana ya "katikati" maana kuna majira ambako nyota hizo ziko katikati kwenye anga. Jina la Kirabu lilipokewa pia na wanaastronomia wa Ulaya wakati wa karne za kati na kwa matamshi ya kigeni kutoka "i-bt-al-geusa" kuwa "Bet-el-geuse". [1]

Jina la kitaalamu la kisasa ni "Alpha Orionis" (α Orionis) kwa sababu ilionekana kuwa nyota angavu zaidi katika kundiyota yake.[2]. "Betelgeuse" ilikubaliwa na kuthibitishwa na UKIA kuwa jina maalum.[3].

Uangavu na umbali

Ni nyota angavu ya tisa kati ya nyota zote zinazoonekana angani na nyota angavu ya pili kwenye Sayadi (Orion). Uangavu wake unachezacheza kati ya vipimo vya 0.2 na 1.2.[4]

Umbali wake na dunia ulikadiriwa mnamo mwaka 2008 kuwa miakanuru 640[5]

Hali ya nyota

Umri wa Ibuti la Jauza haukutimiza miaka milioni 10 lakini umeendelea haraka kutokana na masi yake kubwa. [6]

Ibuti la Jauza imeshaendelea kufikia ngazi za mwisho za mageuzi ya nyota (stellar evolution). Katika kipindi cha miaka milioni 1 ijayo inakadiriwa kutimiza mageuzi yake hadi kulipuka kama nyota nova. [7]

Tazama pia

Marejeo

  1. Jan Knappert, "The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations", katika jarida la The Indian Ocean Review, 6-1993, uk 5-7
  2. Hata hivyo Ibuti la Jauza ilipewa jina la "alfa Orionis" katika orodha ya Bayer inayomaanisha ni nyota angavu kushinda nyingine katika kundi la nyota; inawezekana Bayer aliiona wakati iling'aa zaidi, maana mwangaza wake unachezacheza, lakini kwa kawaida Rijili Kantori (Rigel) inang'aa zaidi.
  3. Naming Stars, tovuti ya Umoja wa Kimataifa wa Astronomia (Ukia|UKIA), iliangaliwa Novemba 2017
  4. Davis, Kate (AAVSO Technical Assistant, Web) 2000. Variable star of the month: Alpha Orionis. American Association of Variable Star Observers (AAVSO). [1]
  5. Harper, Graham M. et al. 2008. A new VLA-Hipparcos distance to Betelgeuse and its implications. The Astronomical Journal 135 (4): 1430–40. [2]
  6. Levesque E.M. 2010. The physical properties of red supergiants. Astronomical Society of the Pacific. 425 Hot and Cool: Bridging Gaps in Massive Star Evolution ASP Conference Series: 103. [3]
  7. "Betelgeuse braces for a collision". ESA. 2013-01-22. Iliwekwa mnamo 2013-01-23.


Viungo vya Nje

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  1. Mars and Orion Over Monument Valley Skyscape showing the relative brightness of Betelgeuse and Rigel.
  2. Orion: Head to Toe Breathtaking vista the Orion Molecular Cloud Complex from Rogelio Bernal Andreo.
  3. The Spotty Surface of Betelgeuse A reconstructed image showing two hotspots, possibly convection cells.
  4. Simulated Supergiant Star Freytag's "Star in a Box" illustrating the nature of Betelgeuse's "monster granules".
  5. Why Stars Twinkle Image of Betelgeuse showing the effect of atmospheric twinkling in a telescope.