Brimin Kipruto
Brimin Kipruto (alizaliwa Korkitony, Wilaya ya Keiyo, 31 Julai 1985) ni mwanariadha wa umbali wa wastani wa Kenya.
Alishiriki hasa katika mbio ya 3000m ya kuruka viunzi ambapo muda wake bora kabisa ni dakika 8:04.22.
Katika Mbio za Dunia za Vijana za 2001 mjini Debrecen,Hungaria alikuwa nambari ya pili katika mbio ya 3000m ya kuruka viunzi. Yeye alimaliza masomo yake ya shule ya upili hapo 2003 kutoka Shule ya Sekondari ya Kipsoen. Mwaka uo huo alishiriki katika Mbio ya Vijana ya Afrika nchini Kamerun na akashinda medali ya fedha.Hapo mwaka wa 2004,katika Mbio ya Vijana ya Afrika alishiriki katika mbio ya 1500m badala ya yake ya kawaida na akawa #3.
Ilpofika mwaka wa 2004, baada ya kumaliza # 2 katika majaribio ya Olimpiki ya Kenya,Kipruto(aliyekuwa kijana wa umri wa miaka 19 tu) alishinda medali ya fedha katika Mbio ya Olimpiki ya 2004 katika mbio ya 3000m kuruka viunzi. Katika Mbio ya Mabingwa ya Dunia ya 2005 mjini Helsinki alishinda medali ya shaba katika mbio iyo hiyo ya 3000m. Yeye alimaliza katika nafasi ya tatu tena katika Mbio ya Dunia ya IAAF ya 2005. Katika mwaka wa 2006,alimaliza katika nafasi ya 6 katika fainali ya Mbio ya Dunia,huku akirudia nafasi yake ya 2004.
Katika mwaka wa 2007, yeye alishinda medali ya dhahabu katika mbio ya kuruka viunzi katika Mbio ya Ubingwa,Osaka. Baada ya kuhitimu timu ya Olimpiki ya 2008, kIpruto alishinda medali ya dhahabu katika mbio hiyo. Ingawa katika Mbio ya Mabingwa ya 2009, bingwa mtetezi alikuwa nambari 7 tu.
Hivi sasa anaishi Korkitony na hufanya mazoezi na kundi la Global Sports, Kaptagat karibu na Eldoret chini ya kocha Patrick Sang na Joseph Chelimo.
Matokeo
haririMatokeo katika mashindano
haririMwaka | Shindano | Pahala palipokimbiwa | Tokeo | Maelezo ya ziada |
---|---|---|---|---|
2001 | Mbio ya Vijana ya Dunia | Debrecen, Hungaria | 2 | 2000 m kuruka viunzi |
2003 | Mbio ya Vijana ya Afrika | Garoua, Kamerun | 2 | 3000 m kuruka viunzi |
2004 | Mbio ya Vijana ya Dunia | Grosetto, Uitalia | 3 | 1500m |
Olimpiki 2004 | Athens, Ugiriki | 2 | 3000m kuruka viunzi | |
Mbio ya Vijana ya IAAF | Monte Carlo, Monaco | 6 | 3000 m kuruka viunzi | |
2005 | Mbio ya Vijana ya IAAF | St Etienne, Ufaransa | 37 | Mbio fupi |
Mbio ya Mabingwa | Helsinki, Finland | 3 | 3000m ya kuruka viunzi | |
Mbio ya Dunia ya IAAF | Monte Carlo, Monaco | 3 | 3000 m kuruka viunzi | |
2006 | Mbio ya Dunia ya IAAF | Fukuoka, Ujapani | 18 | Mbio fupi |
Mbio ya Dunia ya IAAF | Stuttgart, Ujerumani | 6 | 3000 m kuruka viunzi | |
2007 | Mbio ya Dunia ya Mabingwa | Osaka, Ujapani | 1 | 3000m kuruka viunzi |
Mbio ya Dunia ya IAAF ya Fainali | Stuttgart, Ujerumani | 3 | 3000 m kuruka viunzi | |
2008 | Olimpiki ya 2008 | Beijing, Uchina | 1 | 3000m kuruka viunzi |
Mbio ya Dunia ya IAAF ya Fainali | Stuttgart, Ujerumani | 9 | 3000 m kuruka viunzi | |
2009 | Mbio ya Dunia ya Mabingwa | Berlin, Ujerumani | 7 | 3000m kuruka viunzi |
Mbio ya Dunia ya IAAF ya Fainali | Thessaloniki, Ugiriki | 6 | 3000 m kuruka viunzi |
Muda bora(wa kibinafsi)
hariri- 1500m - 3:35.23 (2006)
- 3000m - 7:47.33 (2006)
- 2000m - 5:36.81 (2001)
- 3000m - 8:02.89 (2007)
Viungo vya nje
hariri- IAAF Ilihifadhiwa 3 Septemba 2009 kwenye Wayback Machine.
- Brimin Kipruto kwenye IAAF Ilihifadhiwa 3 Septemba 2009 kwenye Wayback Machine.