Bundi (Tytonidae)
Bundi | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
|
Bundi (pia mabundi) ni ndege mbuai wa familia Tytonidae na jenasi mbalimbali ya familia Strigidae. Ukurasa huu unahusu familia Tytonidae. Spishi hizi zina rangi ya kahawa nyuma na nyeupe mbele pamoja na madoa madogo meusi. Kichwa chao kina umbo la mviringo na uso mwao una umbo la moyo. Bundi hula ndege na wanyama wadogo, wanyama wagugunaji hasa, lakini wadudu wakubwa pia. Jike huyataga mayai 2-7 kwa mahali palipofunika kama tago lililoachwa na ndege mwingine ndani ya tundu ya mti, ufa wa mwamba, dari la nyumba au kihenge n.k.
Mwenendo
haririBundi huwinda usiku na hupumzika mchana. Wanamlenga mbuawa wao kwa msaada ya masikio yao. Manyoya ya uso yapeleka mawimbisauti kwa vipenyo vya masikio viliopo mahali tofauti kidogo kimoja kuliko kingine. Hivyo wanaweza kumkamata mbuawa bila kumwona. Mbuawa hawezi kumsikia bundi akija, kwa sababu mabawa ya bundi hayafanyi sauti yo yote kwa kuwa kingo ya mbele ya manyoya ya mabawa imekerezekakerezeka na ile ya nyuma ina matamvua. Hii inapunguza vurugu ya hewa na kwa hivyo uvumi.
Msambao
haririFamilia hii inayosambaa kwenye eneo pana, ingawa haipo katika kaskazini mwa Amerika ya Kaskazini, Sahara ya Afrika na maeneo makubwa ya Asia. Wanaishi katika makazi mengi kutoka jangwa hadi misitu na kutoka kanda za wastani hadi za tropiki. Nyingi za spishi ishirini zilizopo bado za bundi hazijulikani sana. Baadhi, kama bundi mwekundu, wameonekana kwa nadra au kutafitiwa kidogo tu tangu uvumbuzi wao, kinyume na bundi-mabanda ambaye ni mojawapo ya spishi maarufu za bundi duniani. Hata hivyo, nususpishi kadhaa za bundi-mabanda hustahili kuwa spishi tofauti, lakini hazijulikani sana.
Spishi za Afrika
hariri- Phodilus prigoginei, Bundi wa Kongo (Congo Bay Owl)
- Tyto alba, Bundi-mabanda (Western Barn Owl)
- Tyto a. alba, Bundi-mabanda Kaskazi
- Tyto a. detorta, Bundi wa Kabo Verde
- Tyto a. hypermetra, Bundi wa Kabo Verde
- Tyto a. poensis, Bundi Babawatoto au Babewana
- Tyto a. thomensis, Bundi wa Sao Tome
- Tyto capensis, Bundi-mbuga (African Grass Owl)
- Tyto soumagnei, Bundi Mwekundu (Red Owl)
Spishi za mabara mengine
hariri- Phodilus assimilis (Sri Lanka Bay Owl)
- Phodilus badius (Oriental Bay Owl)
- Tyto alba (Western Barn Owl)
- Tyto a. alba (Southwest European Barn Owl)
- Tyto a. erlangeri (Middle East Barn Owl)
- Tyto a. ernesti (Corsica Barn Owl)
- Tyto a. gracilirostris (Canary Barn Owl)
- Tyto a. guttata (Central European Barn Owl)
- Tyto aurantia (Golden Masked Owl)
- Tyto deroepstorffi (Andaman Masked Owl)
- Tyto furcata (American Barn Owl)
- Tyto glaucops (Ashy-faced Owl)
- Tyto inexspectata (Minahassa Masked Owl)
- Tyto javanica (Eastern Barn Owl)
- Tyto longimembris (Eastern Grass Owl)
- Tyto manusi (Manus Masked Owl)
- Tyto multipunctata (Lesser Sooty Owl)
- Tyto nigrobrunnea (Taliabu Masked Owl)
- Tyto novaehollandiae (Australian Masked Owl)
- Tyto novaehollandiae troughtoni (Cave-nesting Masked Owl) – udhabiti si hakika, yamkini imekwisha (miaka 1960)
- Tyto rosenbergii (Sulawesi Masked Owl)
- Tyto rosenbergii pelengensis (Peleng Masked Owl) - yamkini imekwisha (kati ya karne ya 20)
- Tyto sororcula (Moluccan Masked Owl)
- Tyto (sororcula) cayelii (Buru Masked Owl) – labda imekwisha (kati ya karne ya 20?)
- Tyto tenebricosa (Greater Sooty Owl)
Spishi za kabla ya historia
hariri- Tyto cf. alba/aurantiaca (New Ireland Lesser Barn Owl)
- Tyto balearica (mwisho wa Miocene – kati ya Pleistocene ya Mediteranea)
- Tyto cavatica (Puerto Rican Barn Owl) – labda iliishi bado mwaka wa 1912; labda spishi ndogo ya T. glaucops
- Tyto jinniushanensis (Pleistocene ya Jing Niu Shan, China)
- ?Tyto letocarti (New Caledonian Barn Owl)
- Tyto melitensis (Maltese Barn Owl) – zamani katika jenasi Strix, labda spishi ndogo ya Tyto alba
- Tyto mourerchauvireae (kati ya Pleistocene ya Sisilia, Mediteranea)
- Tyto noeli (Noel's Barn Owl, Kuba)
- Tyto cf. novaehollandiae (Mussau Barn Owl)
- Tyto cf. novaehollandiae (New Ireland Greater Barn Owl)
- Tyto ostologa (Hispaniolan Barn Owl)
- Tyto pollens (Bahaman Barn Owl) – labda iliishi mpaka karne ya 16
- Tyto riveroi (Rivero's Barn Owl, Kuba)
- Tyto robusta (mwisho wa Miocene/mwanzo wa Pliocene ya Rasi ya Gargano, Italia)
- Tyto (robusta) gigantea (mwisho wa Miocene/mwanzo wa Pliocene ya Rasi ya Gargano, Italia)
- Tyto sanctialbani (kati – mwisho wa Miocene ya Ulaya wa Kati) – zamani katika jenasi ya Strix
- Tyto sp. (Cuban Barn Owl)
- Tyto sp. (Barbuda Barn Owls, Barbuda na yamkini Antigua) – angalau spishi 2
Picha
hariri-
Bundi babawatoto
-
Bundi-mbuga
-
Sri Lanka bay owl
-
Oriental bay owl
-
Southwest European barn owl
-
Central European barn owl
-
Andaman masked owl
-
American barn owl
-
Ashy-faced owl
-
Eastern barn owl
-
Eastern grass owl
-
Lesser sooty owl
-
Australian masked owl
-
Sulawesi masked owl
-
Greater sooty owl