Buyagu ni kata ya Wilaya ya Sengerema katika Mkoa wa Mwanza, Tanzania. Msimbo wa posta ni 33333.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 12,306 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 15,483 waishio humo.[2]

Shughuli wanazofanya wakazi wa kata ya Buyangu ni kilimo, ufugaji na uvuvi.

Kilimo wanachojishughulisha nacho ni kile cha kujikimu cha mazao ya chakula kama mihogo, viazi, mahindi, mpunga, mtama, maharagwe na mazao mengine. Kilimo cha biashara ni cha zao la pamba, ambayo inalimwa katika vijiji vyote vinavyounda kata hiyo. Zao hilo limezidi kurudi nyuma kulingana na kushuka kwa bei ya pamba pamoja na kupanda kwa gharama za pembejeo za kilimo hicho. Pia kushuka kwa uzalishaji wa kilimo hicho kunatokana na kufungwa kiwanda cha Buyagu Ginnery iliyokuwa inanunua na inachambua pamba katika maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya kata hiyo.

Uvuvi ni miongoni mwa kazi zinazofanywa na wakazi wa kata hiyo; shughuli hizo zinafanyika katika Ziwa Viktoria, nazo huwasaidia kwa biashara ya samaki na mboga.

Marejeo hariri

  Kata za Wilaya ya Sengerema - Mkoa wa Mwanza - Tanzania  

Bitoto | Busisi | Buyagu | Buzilasoga | Chifunfu | Ibisabageni | Ibondo | Igalula | Igulumuki | Kagunga | Kahumulo | Kasenyi | Kasungamile | Katunguru | Kishinda | Mission | Mwabaluhi | Ngoma | Nyamatongo | Nyamazugo | Nyamizeze | Nyampande | Nyampulukano | Nyatukara | Sima | Tabaruka

  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mwanza bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Buyagu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.