Dioksidi kabonia

(Elekezwa kutoka CO2)

Dioksidi kabonia (pia: dioxidi ya kaboni, pia kabonidayoksidi[1], hewa ukaa, gesi ya ukaa) ni kampaundi inayounganisha atomi mbili za oksijeni na atomi moja ya kaboni katika molekuli. Fomula yake ya kikemia ni CO2.

Dioksidi kabonia

Katika mazingira ya kawaida hutokea kama gesi inayoganda kwenye halijoto chini ya -78.5°C. Katika hali ya gesi haina ladha wala harufu.

Dioksidi kabonia ina matumizi mbalimbali, kwa mfano kama gesi katika vinywaji aina za soda na bia, katika kizima moto za kupambana na moto penye umeme na mengine mengi.

Dioksidi kabonia inatokea wakati viumbehai wanapumua na kutoa pumzi; inatokea zaidi wakati wa kuchoma maada ogania yaani mada yenye kaboni ndani yake. Mimea inahitaji gesi hii kwa mchakato wa usanisinuru inamojenga chakula chao. Inabadilisha CO2 kuwa sukari aina za glukosi.

Athari katika ekolojia

hariri

Kiasi cha kaboni dioksidi hewani imeongezeka katika miaka 150 iliyopita kutokana na kuchoma kwa fueli kisukuku kama makaa mawe na mafuta ya petroli. Uchumi wa viwanda, uzalishaji umeme na usafiri kwa magari yenye Injini mwako ndani kumeleta kuchomwa kwa kiasi kikubwa cha fueli hizi ambazo zote zina kaboni ndani inayomwagwa sasa kwenye angahewa kwa umbo la dioksidi kabonia.

Kuongezeka kwa gesi hii hewani kunasababisha kupanda kwa halijoto duniani kunakoonekana kama tatizo kubwa kwa wakati ujao. Muhimu ni tabia ya CO2 kupitisha nuru inayoonekana kama nuru ya jua lakini kuzuia mnururisho wa infraredi yaani joto. Maana yake nishati ya mwanga unaoonekana inaingia katika angahewa ya dunia lakini joto peke yake halitoki kwa urahisi. Tabia hii ni muhimu kwa uhai duniani kwa sababu kaboni dioksidi hewani inazuia kupoa kwa dunia wakati wa usiku; ila tu kuongezeka kwa gesi kutokana na shughuli za binadamu kunasababisha pia kupanda kwa halijoto duniani na matokeo yake yasiyotakiwa.

Soma pia

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dioksidi kabonia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  1. dioksidi kabonia ni pendekeo la KAST, dioksidi ya kaboni ya TUKI-ESDD3, kabonidayoksaidi ya TUKI-KKS,