Charbel Makhluf, O.L.M. (kwa Kiarabu: مار شربل, ; aliitwa kwanza Youssef Antoun Makhlouf; Bekaa Kafra, Lebanon 8 Mei 1828 – Annaya, Lebanon, 24 Desemba 1898) alikuwa mmonaki halafu pia padri wa Kanisa la Wamaroni katika Shirika la Kilebanoni la Kimaroni.

Mt. Charbel Makhlouf.

Kisha kuishi kikamilifu monasterini, akitamani maisha magumu ya upwekeni na ukamilifu wa juu zaidi, alikubaliwa kuacha jumuia yake aende kuishi peke yake, alipomtumikia Mungu usiku na mchana miaka 23 kwa kujinyima karibu kila kitu, akifunga na kusali hadi kifo chake [1].

Papa Paulo VI alimtangaza mwenye heri tarehe 5 Desemba 1965, halafu mtakatifu tarehe 9 Oktoba 1977.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 24 Julai[2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.