Kanisa la Wamaroni
Kanisa la Wamaroni (kwa Kilatini Ecclesia Maronitarum; jina rasmi: Kanisa la Kisirya la Kimaroni la Antakya; kwa Kiaramu ܥܕܬܐ ܣܘܪܝܝܬܐ ܡܪܘܢܝܬܐ ܕܐܢܛܝܘܟܝܐ ʿīṯo suryaiṯo māronaiṯo d'anṭiokia; kwa Kiarabu الكنيسة الأنطاكية السريانية المارونية al-kanīsa al-antākīyya al-seryānīyya al-mārwnīyya) ni moja ya Makanisa Katoliki ya Mashariki, yaani ni Kanisa linalojitegemea kisheria ndani ya umoja wa Kanisa Katoliki.
Historia
haririMzizi wake ni katika Kanisa la Kisirya la Kiorthodoksi kwenye nchi za Syria na Lebanoni za leo, kwa hiyo katika utamaduni wa Wakristo waliotumia lugha ya Kiaramu cha magharibi.
Kanisa hilo lilianza katika mvutano juu ya maamuzi ya Mtaguso wa Kalsedonia wa mwaka 451 yaliyokataliwa na Wasirya wengi. Wafuasi wa mmonaki Maroni, mwanzilishi wa monasteri maarufu katika karne ya 4, walisimama upande wa maazimio ya huo mtaguso mkuu ingawa walikuwa Wasirya. Kwa hiyo Wamaroni waliteswa na wenzao wakawa kundi la Wasirya waliosimama upande wa Kanisa la Kigiriki la Kiorthodoksi.
Katika mabishano yaliyofuata ndani ya Kanisa la Kigiriki Wamaroni waliamua kukaa kando, wakawa jumuiya ya pekee na kutafuta hifadhi yao kwenye milima ya Lebanoni.
Wakati wa vita vya msalaba Wamaroni walielewana vizuri na Wakatoliki kutoka Ulaya wakatafuta ushirikiano nao. Hapo walikubali uongozi wa Papa wa Roma na kuwa hadi leo Kanisa pekee la Ukristo wa Mashariki lililopo lote chini ya Papa.
Hali ya leo
haririWamaroni wanatunza liturujia, teolojia na maisha ya kiroho ya mazingira hayo kulingana na tapo lililoanzishwa na Maroni. Hadi leo sehemu za liturujia ziko kwenye lugha ya Kisirya au Kiaramu cha magharibi lakini kwa jumla Kanisa na pia jumuiya ya Wakristo wake hutumia Kiarabu.
Patriarki wake anachaguliwa na Sinodi ya maaskofu wa Kanisa hilo, halafu anamuomba Papa wa Roma ushirika kamili. Anaishi Bkerke (Lebanoni), ambapo ana jimbo lake, ingawa anatumia bado jina rasmi la Patriarki wa Antiokia.
Kanisa hilo linakubali kuwapa upadri waamini waliokwishaoa.
Uenezi
haririHuko Lebanoni, ni kundi kubwa, ingawa wanazidi kupungua kwa sababu ya matatizo yanayowafanya wengi kuhamia nchi nyingine.
Wanakaribia kuwa 3,500,000 duniani kote [1], wakiishi katika majimbo 28 kama yafuatavyo.
Huko Lebanoni: Zahleh, Tiro, Tripoli, Sidoni, Joubbeh - Sarba - Jounieh (jimbo la Patriarki), Jbeil - Byblos, Beirut, Batrun, Baalbeck - Deir el Ahmar na Antelias
Huko Syria: Latakia, Damascus na Aleppo.
Huko Israel: Haifa - Nchi Takatifu.
Katika nchi nyingine: Afrika Magharibi na ya Kati (Ibadan, Nigeria), Brooklyn (Marekani), Buenos Aires (Argentina), Cairo (Misri), Cyprus, Kolombia, Los Angeles (Marekani), Mexico, Montreal (Canada), Paris (Ufaransa), Sao Paulo (Brazil), Sudan na Sydney (Australia).
Tanbihi
haririMarejeo
hariri- Moosa, Matti, The Maronites in History, Gorgias Press, Piscataway, NJ, 2005, ISBN 978-1-59333-182-5
- R. J. Mouawad, Les Maronites. Chrétiens du Liban, Brepols Publishers, Turnhout, 2009, ISBN 978-2-503-53041-3
- Kamal Salibi - A House of Many Mansions - The History of Lebanon Reconsidered (University of California Press, 1990).
- Maronite Church. New Catholic Encyclopedia, Second Edition, 2003.
- Riley-Smith, Johnathan - The Oxford Illustrated History of the Crusades (Oxford University Press, Oxford, 1995)
Viungo vya nje
hariri- Maronite History Project Ilihifadhiwa 2 Julai 2009 kwenye Wayback Machine. — a Maronite encyclopedia wiki
- The Druzes and the Maronites under the Turkish Rule from 1840 to 1860 Cornell University Library Historical Monographs Collection.
- Catholic Culture: News — Maronite population discussed
- Tovuti rasmi ya Kanisa la Wamaroni Ilihifadhiwa 29 Desemba 2016 kwenye Wayback Machine.
- Orodha ya majimbo ya Kanisa la Wamaroni
- Maronite Rite diocese based in Sydney, Australia
- Eparchy of Saint Maron of Brooklyn
- Eparchy of Our Lady of Lebanon Ilihifadhiwa 30 Machi 2019 kwenye Wayback Machine.
- Congregation of the Lebanese Maronites Missionnaries Ilihifadhiwa 27 Julai 2011 kwenye Wayback Machine.
- The Maronite Monks of Adoration, Most Holy Trinity Monastery Ilihifadhiwa 7 Novemba 2008 kwenye Wayback Machine. — monastery in Massachusetts
- Hati Orientalium Ecclesiarum ya Mtaguso wa pili wa Vatikano
- Hati Orientales omnes Ecclesias ya Papa Pius XII
- [1] Ilihifadhiwa 5 Machi 2012 kwenye Wayback Machine. - Hati ya Papa Yohane Paulo II Orientale Lumen kuhusu Makanisa ya Mashariki
- Codex Canonum Ecclesiarum Orientalium - Mkusanyo wa Sheria za Makanisa ya Mashariki (katika Kilatini pamoja na sehemu sambamba)
- Instruction for Applying the Liturgical Prescriptions of the Code of Canons of the Eastern Churches Ilihifadhiwa 25 Aprili 2009 kwenye Wayback Machine. - Hati ya Idara ya Papa kwa Makanisa ya Mashariki kuhusu liturujia
- Ujuzi wa msingi kuhusu Makanisa hayo Ilihifadhiwa 17 Mei 2011 kwenye Wayback Machine.
- CNEWA Idara ya Papa inayosaidia Makanisa hayo Ilihifadhiwa 9 Machi 2009 kwenye Wayback Machine.
- Sura ya Idara ya Papa kwa Makanisa hayo
- Takwimu za Makanisa Katoliki ya Mashariki
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kanisa la Wamaroni kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |