DP World ni kampuni ya kimataifa ya Emirati inayojihusisha na usafirishaji iliyoko Dubai, Falme za Kiarabu. Imejikita na usafirishaji wa mizigo, shughuli za bandari, huduma za baharini na maeneo ya biashara huria. Iliundwa mwaka 2005 kwa muunganiko wa mamlaka ya bandari ya Dubai (Dubai Ports Authority) na mamlaka ya bandari ya Dubai kimataifa (Dubai Ports International), DP World inashughulikia makontena milioni 70 ambayo huletwa na karibu meli 70,000 kila mwaka. Hii ni sawa na takriban 10% ya makontena yanayosafirishwa ya kimataifa yanayotolewa na vituo vyao 82 vya baharini na nchi kavu vilivyopo katika zaidi ya nchi 40. Hadi mwaka 2016, DP World ndiyo kampuni iliyokuwa ikiendesha bandari kimataifa, na tangu wakati huo, imepata na kushirikiana na makampuni mengine juu na chini ya mnyororo wa thamani.

DP World

Historia

hariri

Zamani

hariri

Dubai Ports International (DPI) ilianzishwa mwaka 1999. [1] Mradi wake wa kwanza ulikuwa huko Jeddah, Saudi Arabia, akishirikiana na mshirika wa ndani kwenye South Container Terminal (SCT). DPI kisha iliendelea na kuendeleza shughuli katika bandari za Djibouti mwaka wa 2000, Vizag, India mwaka 2002 na Constanta, Romania mwaka 2003. [1] Mnamo Januari 2005, DPI ilipata vituo duniani vya CSX (CSX WT). [2] Baadaye Septemba 2005 ndipo Dubai Ports International iliunganishwa rasmi na mamlaka ya bandari ya Dubai kuunda DP World. [3] Upanuzi wa haraka kupitia ununuzi uliendelea Machi 2006 wakati DP World ilinunua kampuni ya nne kubwa zaidi ya waendeshaji bandari duniani, P&O kwa £3.9 bilioni.

2006: Mzozo wa usalama wa bandari ya Marekani

hariri

Umiliki wa aina mbalimbali za bandari Marekani na DP World ( kama sehemu ya mkataba wa P&O) ilionekana kuwa yenye utata na wengi nchini Marekani ingawa iliungwa mkono na Rais wa Marekani George W. Bush ; bandari za Marekani ziliuzwa muda mfupi baadaye.

P&O iliendesha kampuni kuu za Marekani New York, New Jersey, Philadelphia, Baltimore, New Orleans, na Miami . Kabla ya makubaliano hayo kupatikana, mpango huo ulipitiwa upya na Kamati ya Uwekezaji wa Kigeni nchini Marekani inayoongozwa na Idara ya hazina ya Marekani na zikiwemo Idara za nchi, biashara na Usalama wa Taifa . Ilipewa mwanga wa kijani ilikuendelea na shughuli zake, lakini muda mfupi baadaye, wanachama wote wa Democratic na Republican wa Congress walionyesha wasiwasi juu ya athari mbaya ambayo mpango huo ungekuwa nayo kwa usalama wa bandari.

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 "About DP World – History". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 5 Novemba 2012. Iliwekwa mnamo 2012-11-27.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. International, CSX Corporation; Dubai Ports. "Dubai Ports International Completes Acquisition Of CSX World Terminals". www.prnewswire.com. Iliwekwa mnamo 13 Novemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  3. "Dubai merger sees world's largest port operation". 29 Septemba 2005. Iliwekwa mnamo 13 Novemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)