Daraja la Rusumo

Daraja la Rusumo ni daraja la kimataifa linalovuka Mto Kagera na kuunganisha nchi jirani za Rwanda na Tanzania.

Daraja la Rusumo
Kiingereza: Rusumo Bridge
YabebaBarabara kuu ya B3 (leni 1)
YavukaMto Kagera
Urefumita 100
Upanamita 3.5
Kiasi cha mzigotani 8
Yafuatiwa naDaraja la Kyaka
Anwani ya kijiografia2°22′56.35″S 30°46′59.64″E / 2.3823194°S 30.7832333°E / -2.3823194; 30.7832333
Daraja la Rusumo is located in Tanzania
Daraja la Rusumo
Mahali ya daraja nchini Tanzania

Daraja la kaleEdit

Daraja la kwanza ni feleji lenye urefu wa mita 64 lililotengenezwa huko Torino nchini Italia kuanzia mwaka 1966, kusafirishwa hadi Tanzania na kuunganishwa mahali pake mwaka 1972.

Tarehe 28 Aprili 1994, wakati wa mauaji ya kimbari ya Rwanda, zaidi ya wakimbizi 200,000 walipitia daraja hilo katika muda wa masaa 24. [1]

Kutokana na kuongezeka kwa usafiri wa kupitia daraja hilo, halikutosha tena, hasa kwa sababu ni jembamba: kuna njia moja pekee kwa magari. Vilevile lilikadiriwa kubeba tani 56 ambazo ni uzito unaopitiwa na malori makubwa. Hivyo mpango wa kujenga daraja jipya ulianzishwa mwaka 2012.

Daraja jipyaEdit

Daraja la pili la Rusumo lilikamilishwa kando ya daraja la kale kwenye mwaka 2014. Daraja hilo lilijengwa na kampuni ya Japani ya Daiho Corporation Company[2]. Daraja lilitengenezwa vipandevipande huko Japani, kupelekwa Dar es Salaam na kusafirishwa hadi Rusumo ambako vipande viliunganishwa.

Daraja jipya huwa na njia mbili za magari likiwa na uwezo wa kubeba tani 400 kwa wakati mmoja.[3]

MarejeoEdit

  1. Issue 110 (Crisis in the Great Lakes) - Cover Story: Heart of Darkness. UNHCR (1 December 1997). Iliwekwa mnamo 27 December 2014.
  2. Rusumo Bridge construction starting soon, E-newsletter Vol. 1 April – June 2012, tovuti ya Japan International Cooperation Agency, iliangaliwa Februari 2020
  3. The Bridge at Rusumo, tovuti ya Japan International Cooperation Agency, iliangaliwa Februari 2020