Katekisimu ya Kanisa Katoliki
Katekisimu ya Kanisa Katoliki (kwa kifupi KKK) ni kitabu rasmi cha kufundishia dini ya Ukristo kadiri ya imani na maadili ya Kanisa Katoliki kutokana na Mtaguso wa pili wa Vatikano.
Ilikubaliwa na Papa Yohane Paulo II kwanza tarehe 11 Oktoba 1992, halafu moja kwa moja 15 Agosti 1997.
Katika mtandao inapatikana katika lugha zifuatazo:
Vitabu vilivyotangulia
haririVitabu vya kufundishia dini ya Kikristo vilitolewa kuanzia Mababu wa Kanisa, lakini neno maalumu katekisimu lilianza kutumiwa na Martin Luther mwaka 1529.
Wakati wa Mtaguso wa Trento ilitolewa katekisimu kwa ajili ya maparoko ili waweze kufundisha vizuri imani katoliki. Katekisimu ya Trento ilipitishwa na Papa Pius V ikaenea katika Kanisa Katoliki lote.
Baada yake, hakukuwa na katekisimu nyingine ya kimataifa, ingawa kuanzia mwaka 1905 ilienea sana ile iliyoandikwa na Papa Pius X kwa jimbo la Roma.
Walengwa
haririKatekisimu ya Kanisa Katoliki inatarajiwa kutumika hasa kama msingi kwa utunzi wa katekisimu za kila lugha na aina kadiri ya mahitaji ya watu.
Yaliyomo
haririKatekisimu ya Kanisa Katoliki ina sehemu kuu nne:
- Ungamo la imani (ufafanuzi wa Kanuni ya imani ya mitume)
- Adhimisho la fumbo la Kikristo (liturujia na hasa sakramenti saba)
- Maisha ya Kikristo (maadili yakitegemea Amri za Mungu)
- Sala ya Kikristo (hasa ile ya Baba Yetu)
Mafundisho yote yanaendana na madondoo mengi, hasa ya Biblia, Mababu wa Kanisa, Mitaguso ya kiekumene, Mapapa na watakatifu.
Ufupisho Makini
haririPapa Benedikto XVI, ambaye alipokuwa kardinali (Joseph Ratzinger) aliongoza utunzi wa KKK, mwaka 2005 alitoa Ufupisho wake, uliotafsiriwa katika Kiswahili kwa jina la Ufupisho Makini.
Katika mtandao anapatikana kwa lugha mbalimbali, k. mf. kwa Kiingereza: Compendium of the Catechism of the Catholic Church