Dominiko wa Calzada

Dominiko wa Calzada (jina la kuzaliwa kwa Kihispania: Domingo Garcia; Burgos, Castilia Mpya, Hispania, 1019 hivi - Santo Domingo de la Calzada, Hispania, 12 Mei 1109[1]) alikuwa padri mkaapweke aliyehudumia hadi kifo chake waumini walioelekea Santiago de Compostela kwa hija[2].

Sanamu yake katika kanisa kuu la mji uliotokea kando ya nyumba yake.

Kabla ya hapo alijaribu kujiunga na monasteri mbalimbali akakataliwa kwa sababu ya ulemavu wa viungo vyake na udogo wa akili yake[3].

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 12 Mei[4].

Tazama piaEdit

TanbihiEdit

Viungo vya njeEdit

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.