Donasiani na Rogasiani

Donasiani na Rogasiani (walifariki Nantes, Galia, Ufaransa wa leo, 24 Mei 304) walikuwa ndugu waliouawa kwa ajili ya imani yao wakati wa dhuluma ya Dola la Roma[1][2].

Sanamu za Wat. Donasiani na Rogasiani (P. Potet, 1850), Paris.

Donasiani alikuwa ameshabatizwa, na ndiye aliyemuinjilisha kaka yake. Walipohukumiwa kufa, Rogasiani alionyesha sikitiko lake la kufa bila ubatizo, lakini mdogo wake alimfariji kwamba damu yake itamtakasa vilevile. Basi, wakachomwa kwa mkuki na kukatwa kichwa.

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 24 Mei[3]

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.