Ukame

(Elekezwa kutoka Drought)

Ukame (kwa Kiingereza "Drought") ni hali ya hewa ya sehemu au mahali fulani inayofanya pakose maji ya kutosha kwa muda mrefu[1]. Kwa kawaida hii inamaanisha kipindi ambako kuna mvua kidogo, au kupungukiwa kwa usimbishaji mwingine kama theluji.

Nyufa katika ardhi kutokana na ukame (Sonoran desert, Mexico).

Ukame unatokea pia pale ambako watu na kilimo wanategemea maji kwa umwagiliaji na vyanzo vingine vya maji vinakauka.

Ukame unaweza kuhatarisha uhai wa mimea, wanyama na watu, ambao wote wanahitaji maji.

Matokeo ya ukame

hariri
  • hakuna maji ya kutosha kwa wakazi wa eneo fulani.
  • mavuno yanapungua, bei za mazao yanapanda
  • lishe ya wanyama inapungua, bei za nyama, maziwa na bidhaa nyingine zinazotokana na wanyama zinapanda
  • usafirishaji wa bidhaa kwenye njia za maji unapata matatizo kama maji mtoni na miferejini yanapungua mno
  • uzalishaji wa umememaji unapungua kama hakuna maji ya kutosha tena kuendesha rafadha
  • vituo vya umeme na viwanda ambavyo vinategemea maji ya mito kwa kupoza mashine zao haziwezi kuendelea kwa nguvu; kiasi cha maji kinachopatikana kinapungua, na maji hayo yanakuwa na halijoto ya juu zaidi, kwa hiyo uwezo wa kupoza injini inapungua
  • hatari ya moto kwenye misitu na porini
  • kukausha kwa mimea inaacha ardhi bila kinga, mmomonyoko unaongezeka
  • dhoruba itabeba kiasi kikubwa cha mchanga na vumbi kwenye angahewa, hivyo kupeleka ardhi yenye rutuba penginepo na kuongeza magonjwa ya mfumo wa upumuaji kutokana na vumbi hewani.

Tanbihi

hariri
  Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.