Edward Steere
Edward Steere (1828 - 26 Agosti 1882) alikuwa mwanatheolojia Mwanglikana kutoka Uingereza aliyepata kuwa askofu wa Zanzibar akikumbukwa kuwa kati ya Wazungu wa kwanza waliokusanya matini za Kiswahili na kutunga sarufi ya lugha hiyo. [1]
Edward Steere | |
Amekufa | 26 Agosti 1882 |
---|---|
Kazi yake | mwanatheolojia] |
Cheo | Askofu |
Maisha
haririSteere alisoma theolojia kwenye Chuo Kikuu cha London akabarikiwa mnamo 1850. [2] Baada ya kuhudumia kama mchungaji huko Devon na Lincolnshire, alijiunga na William Tozer (Askofu Mwanglikana wa Afrika ya Kati) kwenye safari ya kwenda Unyasa mnamo 1863. [3] Aliteuliwa Askofu wa Afrika ya Kati [4] mnamo 1874 akaaga dunia mnamo 26 Agosti 1882. [5]
Edward Steere alikaa miaka mingi kule Zanzibar, 1864-1868, 1872-1874, na 1877-1882. Mnamo 1873 aliweka jiwe la msingi katika Kanisa la Christ Church, Zanzibar, katika Mji Mkongwe wa Unguja. Alishiriki katika ubunifu wa kanisa hilo lililojengwa mahali pa soko la watumwa la awali. Steere alishirikiana pia na David Livingstone kwa lengo la kumaliza utumwa huko Zanzibar. Amezikwa nyuma ya madhabahu kwenye kanisa. [6]
Mnamo mwaka 1875 alianzisha shirika lifaamikalo kama "The East Africa Church Missionary Society" (EACMS) ambalo lilitoa mafunzo kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Askofu Edward Steere pamoja na shirika lake waliweza kuanzisha kamusi mbalimbali. Kwa uzuri zaidi shirika hilo ndilo lililosanifisha lugha ya Kiswahili mnamo mwaka 1930.
Mtafiti wa lugha
haririSteere alikuwa mtaalamu mkubwa wa lugha akatoa vitabu kadhaa kuhusu lugha mbalimbali za Afrika Mashariki, zikiwa pamoja na Kishambala, Kiyao, Kinyamwezi, na Kimakonde. Lakini anafahamika zaidi kwa utafiti wake kuhusu Kiswahili. Alitunga "Handbook of Swahili" (Mwongozo wa Kiswahili) mnamo 1870, alipojumlisha sarufi pamoja na kamusi ndogo. Pia alikusanya masimulizi aliyosikia Unguja (Swahili Tales) na kutafsiri sehemu kubwa ya Biblia. [7] Mwanafunzi wake A.C. Madan alitumia kazi ya Steere alipoendelea kutunga kamusi za Kiswahili-Kiingereza na Kiingereza-Kiswahili zilizokuwa kamusi sanifu kwa miaka mingi.
Vitabu alivyotunga
hariri- Steere, Edward. 1869. Anjili ya Bwana Wetu na Mwokozi Wetu Isa Masiya kwa
Mattayo. Maneno ya Kiswahili. London.
- Steere, Edward. 1870. Handbook of the Swahili Language, as spoken at Zanzibar.
London. Bill & Dadly. (B.8.17.11.).
- Steere, Edward. 1876. On the Use of Arabic Alphabet in Swahili. UMCA.
- Steere, Edward. 1882. Swahili Exercises Compiled for the Universities´ Missions to
Central Africa. London.
- Steere, Edward. 1906. Swahili Tales. London: Bell & Dadly (Revised 1922: London, SPCK
Tanbihi
hariri- ↑ Zanzibar Christians
- ↑ The Times, Tuesday, Aug 29, 1882; pg. 6; Issue 30598; col D Obituary
- ↑ Heanley, R. M. A Memoir of Edward Steere, D.D. Ll.D., Third Missionary Bishop in Central Africa. (see External links).
- ↑ Ranger, Terence O.; Kimambo, Isaria N. (1976). The Historical Study of African Religion. University of California Press. ISBN 978-0-520-03179-1.
- ↑ The Times, Tuesday, Sep 19, 1882; pg. 4; Issue 30616; col F Bishop Steere And His Work
- ↑ 'Workers at the church'
- ↑ Dictionary of National Biography entry; see External links below.
Marejeo
hariri- "The Bishop Of Grahamstown (sic!) On The Progress Of The Church". Manchester Courier and Lancashire General Advertiser. 13 Agosti 1877. Iliwekwa mnamo 2014-09-07.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) (Steere hakuwa askofu wa Grahamstown, gazeti lilichanganya majina) - "Ecclesiastical Intelligence". Morning Post. 8 Januari 1875. Iliwekwa mnamo 2014-09-07.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Viungo vya nje
hariri- Works by Edward Steere katika Project Gutenberg
- Works by Edward Steere
- Works by or about Edward Steere
- Robert Marshall Heanley (1898) A Memoir of Edward Steere, D.D., LL.D., Office of the Universities' Mission to Central Africa, London (Google ebook)
- Dictionary of National Biography entry Steere, Edward, by C. A. Harris
- Steere's A Handbook of the Swahili Language as spoken at Zanzibar original 1870 edition.
- Steere's A Handbook of the Swahili Language as spoken at Zanzibar revised by A.C. Madan 1894.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |