Kanisa la Kristo, Zanzibar
Kanisa la Kristo (kwa Kiingereza: Christ Church Cathedral) ni kanisa kuu la Anglikana mjini Zanzibar lililo kati ya vivutio vya kihistoria vya mji huo[1]. Liko Mkunazini Road, katikati ya Mji Mkongwe.
Usanifu majengo uliotumika ni kati ya vielelezo vya kwanza vya Usanifu majengo wa Kikristo katika Afrika Mashariki[2]. Umbo la kanisa hilo linaunganisha tabia za ubunifu wa Kizungu, hasa mtindo wa Kigothi, na ubunifu wa Kiislamu, hasa katika mapambo na umbo la madirisha[3][4]. Waanglikana walipenda kuunganisha mbinu hizo katika makanisa waliyojenga katika mazingira ya Kiislamu.
Ujenzi uliongozwa na askofu Edward Steere aliyechagua mahali pa Soko la watumwa lililofungwa mwaka 1873. Mwaka ule Sultani wa Zanzibar alipaswa kuitikia matishio ya serikali ya Uingereza ya kuachana na biashara ya watumwa katika himaya yake. Eneo la soko hilo lilinunuliwa na Mwingereza na kutolewa kama zawadi kwa Steere aliyeanzisha hapa sherehe za ibada[5], kwanza katika kibanda cha muda lakini kwenye sikukuu ya Krismasi 1873 aliweka jiwe la msingi la kanisa[6].
Steere alitumia mahali pa soko hilo kwa jengo jipya kama ishara ya wakati mpya[1]. Alijaribu kuonyesha Ukristo kama dini ya uhuru na kulenga hasa kupokea watumwa katika Ukristo. Altari ilijengwa mahali ilipowahi kusimama nguzo ya kuwafunga watumwa wakati wa kuwapiga viboko[7]. Msalaba ndani ya kanisa ulichongwa kwa ubao wa mti kutoka kijiji cha Chitambo nchini Zambia, mahali ambako David Livingstone aliaga dunia[8].
Ujenzi uliendelea hadi mwaka 1879 ambako kanisa jipya lilizinduliwa rasmi kwenye sikukuu ya Krismasi[9].
Askofu Steere alizikwa katika kanisa hilo baada ya kifo chake kwenye mwaka 1882.
Sasa ni kanisa kuu la dayosisi ya Zanzibar ya Kanisa la Kianglikana. Liliwekwa wakfu mwaka 1903[3]. Kwa sasa linahitaji ukarabati[3].
Picha
haririMarejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 "The Anglican Cathedral Church of Christ". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-08-30. Iliwekwa mnamo 2010-11-22.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help); More than one of|archivedate=
na|archive-date=
specified (help); More than one of|archiveurl=
na|archive-url=
specified (help) - ↑ Zanzibar Christians
- ↑ 3.0 3.1 3.2 The Cathedral Archived Juni 19, 2010, at the Wayback Machine
- ↑ Heanley, R. M.: A memoir of Edward Steere, London 1888, ukurasa 252 (online hapa kwa archive.org)
- ↑ Heanley, ukurasa 119
- ↑ Heanley, uk 121
- ↑ Heanley, uk 252
- ↑ Saint Monica's Tours Archived Mei 2, 2012, at the Wayback Machine
- ↑ Heanley, R. M. (1888). A Memoir of Edward Steere. London: George Bell and Sons. uk. 252.
Viungo vya nje
hariri- Information on the restoration of the cathedral in 2014–15
- The Anglican Cathedral Church of Christ Archived 30 Agosti 2010 at the Wayback Machine., tovuti ya www.zanzibar.cc
- Christ Church Cathedral - the building Archived 28 Juni 2017 at the Wayback Machine.,kwenye tovuti rasmi http://www.zanzibaranglican.or.tz Archived 23 Mei 2021 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kanisa la Kristo, Zanzibar kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |