Egidi mkaapweke

Egidi mkaapweke (kwa Kifaransa Gilles; 650 hivi – 710 hivi) alikuwa mmonaki Mgiriki[1] kutoka Athens, ingawa habari za maisha yake kiini chake ni mikoa ya Provence na Septimania (leo Ufaransa Kusini).

Sehemu ya mchoro wa mwaka 1500 hivi.

Kaburi lake huko Saint-Gilles-du-Gard limekuwa kituo muhimu cha hija kutoka Arles kwenda Santiago de Compostela kumhesimu mtume Yakobo Mkubwa.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Septemba[2].

Tazama piaEdit

TanbihiEdit

  1. Wyschogrod (1990), p. 27; Chaucer and Schmidt (1976), p. 161, Note #632.
  2. Martyrologium Romanum

VyanzoEdit

Viungo vya njeEdit