Emilíana Torrini (alizaliwa 16 Mei 1977) ni mwimbaji na mtunzi wa nyimbo wa Aisilandi. Anajulikana zaidi kwa wimbo wake “Jungle Drum”, albamu yake Love in the Time of science, na onyesho la “The Lord of the Rings: The Two Towers.

Emilíana Torrini akiwa katika tamasha la Furia Sound Festival 2009
Emilíana Torrini katika tamasha la SPOT festival 2009
Emilíana Torrini akiwa Het Paradiso, Amsterdam

Maisha ya awali hariri

Emiliana alizaliwa Aisilandi, na kukulia Kópavogur. Baba yake Salvatore Torrini, Mwitalia (kutoka Naples), wakati mama yake, Anna Stella Snorradóttir, ni Muaisilandi. Kwa sababu ya kanuni ndani ya Aisilandi kwa kipindi hicho, baba yake ingebidi kubadili jina lake na kuwa “ Davíð Eiríksson”, ambayo pia ilimaanisha kwamba Emilíana angetumia jina la ukoo la baba yake kimila. Baada ya miaka kadhaa, kanuni za jina zilibadilishwa,[1] na aliruhusiwa kutumia tena jina lake asilia la ukoo.[2][3] Akiwa na umri wa miaka saba alijiunga na kwaya kama “Soprano”, mpaka alipokwenda shule ya “opera” alipokuwa na umri wa miaka 15. Baada ya kukutwa akiimba kwenye mgahawa ndani ya Aisilandi na Derek Birkett, mmiliki wa One Little Indian Records, Emilíana aliombwa kutembelea London kurekodi wimbo. Aliamua kukaa London.

Kazi hariri

Emilíana alikuwa mwanachama wa kikundi cha kisanaa cha GusGus cha Aisilandi na kuchangia sauti kwenye nyimbo kadhaa katika toleo lao la kwanza Polydistortion (1997), haswa “Why”. Pia alishirikishwa na Kylie Minogue kuandika “Slow” na “Someday” kutoka kwenye album yake ya Body Language mwaka 2003. Pia aliandaa “Slow” akiwa pamoja na Dan Carey; wawili walipendekezwa kuwania kibao bora cha densi tuzo za Grammy mwaka 2005 kwa ajili ya kazi yao kwenye hicho kibao. Hapo awali, Emilíana alichangia sauti kwenye nyimbo za shirika la Thievery mwaka 2002 kwenye album ya The Richest Man in Babylon na kutambuliwa kwa kutunga nyimbo "Resolution", "Until The Morning", na "Heaven's Gonna Burn Your Eyes" kutoka kwenye hiyo album. Pia mwaka 2002, aliimba sauti kwenye wimbo wa Paul Oakenfold "Hold Your Hand" uliyotolewa kwenye album yake ya Bunkka.[4] Mnamo 3 Juni 2013,[5] Emilíana aliweka wazi kwa mashabiki wake kwamba ataachia album yake mnamo 9 Septemba 2013 Uingereza. Album ilitolewa Ayalandi,[6]Aisilandi, Ujerumani, Austria, na Switzerland mnamo 6 septemba 2013. LP mpya inajulikana kama Tookah. Emilíana aliongoza kushiriki katika matamasha ya muziki mpaka album ilipoachiwa Urusi na Budapest. Mnamo 29 Julai 2013, Emilíana alitoa nakala ya redio ya wimbo wake mpya "Speed of Dark".[7] Nyimbo nyingine tatu za nyongeza zikijumuisha "Autumn Sun", "Animal Games", na "Tookah’’ ziliachiwa na kuruhusu mashabika kuzipata.[8] Emiliana alishirikishwa kwenye albamu ya muziki ya Kid Koala ya 2017 kupelekea: Satellite ambapo aliimba nyimbo saba.

Diskografia hariri

  • Crouçie d'où là (1995)
  • Merman (1996)
  • Love in the Time of Science (1999)
  • Fisherman's Woman (2005)
  • Me and Armini (2008)
  • Tookah (2013)

Marejeo hariri

  1. Information. Ministry of the Interior. Jalada kutoka ya awali juu ya 2010-05-05. Iliwekwa mnamo 2021-03-29.
  2. Excerpt in fan forum from an interview by Mark Radcliffe Archived 2011-07-24 at the Wayback Machine at BBC, 17 January 2005
  3. Icelandic names
  4. Paul Oakenfold Feat. Emiliana Torrini – Hold Your Hand. YouTube (2007-09-21).
  5. Archived copy.
  6. Tookah. iTunes.
  7. Kigezo:Cite av media
  8. Tookah Clips. SoundCloud.

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
 
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu: