Nyanda za juu za Ethiopia

(Elekezwa kutoka Ethiopian Highlands)

Nyanda za juu za Ethiopia ni eneo la milima mirefu nchini Ethiopia zikienea hadi Eritrea. Sehemu kubwa za eneo hilo zina kimo za kuanzia mita 1,500 juu ya usawa wa bahari, na vilele vya milima mirefu zaidi vinafikia mita 4,500[1].

Ramani ya Ethiopia.
Milima ya Semien.

Jiografia

hariri

Nyanda za juu zinagawanywa katika sehemu mbili zinazotengwa na Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki.

Upande wa kaskazini-magharibi wa nyanda za juu huwa na majimbo ya Amhara na Tigray pamoja na milima ya Semien. Kilele chake ni Ras Dashen (m 4,550) ambayo ni mlima mrefu wa Ethiopia. Ziwa Tana ambalo ni chanzo cha Nile ya buluu liko pia katika sehemu ya kaskazini magharibi ya Nyanda za Juu za Ethiopia.

Sehemu ya kusini mashariki iko zaidi ndani ya Jimbo la Oromia. Milima ya Bale ni karibu sawa kwa kimo na ile ya Semien. Mlima Tullu Demtu (m 4,337) ni mlima mrefu wa pili nchini Ethiopia.

Miji mikubwa ya nchi iko kwenye mwinuko wa mita 2,000 - 2,500 juu ya usawa wa bahari, ikiwa pamoja na Addis Ababa na miji mikuu ya kihistoria kama vile Gondar na Axum.

Jiolojia

hariri
 
Kaldera ya volkeno Dendi.

Nyanda za juu za Ethiopia zilianza kwenda juu miaka milioni 75 iliyopita wakati magma kutoka koti ya Dunia ilipanda juu. Eneo la miamba iliyopandishwa juu iligawiwa takriban miaka milioni 22–25 iliyopita kwa kutokea kwa Bonde la Ufa. Pamoja na sehemu mbili za milima iliyopo upande wa Afrika, milima kwenye kusini ya Rasi ya Uarabuni ina jiolojia ileile na hivyo ni tawi la nyanda za juu za Ethiopia zilizotengwa leo na ufa mkubwa uliojazwa maji ya Bahari ya Shamu.

 
Nyanda za juu za kaskazini, nyuma Mlima Ras Dashan.

Marejeo

hariri
  1. Paul B. Henze, Layers of Time (New York: Palgrave, 2000), p. 2.

Viungo vya nje

hariri
  • "Ethiopian montane forests" . Jumuia za ulimwengu . Mfuko wa Wanyamapori Ulimwenguni.
  • "Ethiopian montane grasslands and woodlands" . Jumuia za ulimwengu . Mfuko wa Wanyamapori Ulimwenguni.
  • "Ethiopian montane moorlands" . Jumuia za ulimwengu . Mfuko wa Wanyamapori Ulimwenguni.
  • Programu ya Uhifadhi wa Wolf ya Ethiopia
  Makala hii kuhusu maeneo ya Ethiopia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Nyanda za juu za Ethiopia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.