Frédéric Chopin

Mtunzi wa Kifaransa-Kipolishi na mpiga piano

Frédéric Chopin (jina la Kipoland: Fryderyk ; 22 Februari 1810 kulingana na cheti cha kuzaliwa - 17 Oktoba 1849; pengine, tarehe 1 Machi au 10 Machi zimetajwa kama siku yake ya kuzaliwa) alikuwa mtunzi wa Opera na mpigaji kinanda mashuri kutoka nchini Poland. Ni mtunzi muhimu kabisa kwa nchi ya Poland. Ingawaje kuna baadhi ya tungo zake zilikuwa vigumu sana kuzipiga, na zilibahatika kuwa moja kati ya tungo zilizowahi kutungwa vema.

Frédéric Chopin.

Alizaliwa katika kijiji kidogo cha Żelazowa Wola karibu na Warshawa wakati sehemu ile ilikuwa chini ya utawala wa Urusi. Baba alikuwa Nicolas Chopin Mfaransa aliyeishi Poland kama mwalimu na mamake Justyna Krzyżanowska aliyetoka katika familia ya makabaila maskini wa Poland. Frederic alianza mapema kupiga kiananda akaonyesha uwezo mkubwa. Alipofikia umri wa miaka 20 alisafiri Ufaransa alipotoa maonyesho ya muziki yake. 1830 baba alimshauri asirudi Poland kwa sababu ya uasi wa Wapoland dhidi ya utawala wa Kirusi. Baada ya kukandamizwa kwa uasi huu Frederic alibaki nje ya nchi yake ya kuzaliwa akaendelea kuishi na kufanya kazi mjini Paris hasa.

Ni hapa Paris ya kwamba alikuwa maarufu kama mtunga muziki. Alianzisha mapenzi na wanawake mbalimbali lakini hakubahatika kufunga ndoa. Afya yake ilikuwa hafifu muda wote akafa mjini Paris kwa sababu ya ugonjwa wa kifua kikuu mwaka 1849 akiwa na umri wa miaka 39 pekee. Alizikwa Ufaransa lakini moyo wake ulipelekwa Poland na kuzikwa huko katika kanisa mjini Warshawa.

Viungo vya nje

hariri
Wasifu
Tungo za muziki


Baadhi ya rekodi
Mengineyo
 
WikiMedia Commons


Orodha ya Wanamuziki wa kipindi cha Romatiki
Alkan Balakirev Beethoven Bellini Berlioz Berwald Bizet Borodin Brahms Bruckner Chopin Cui Dvořák Elgar Field Franck Glinka Grieg Liszt Mahler Mendelssohn Mussorgsky Rachmaninoff Rimsky-Korsakov Saint-Saëns Schubert Schumann Smetana Strauss Tchaikovsky Verdi Wagner Wolf Weber