Fundumaji
Fundumaji, fudumaji, bwanga, talali au vumba ni aina ya tunda linalotokana na mti mrefu unaoitwa mfundumaji k.m. (Vitex mombassae).
Katika Afrika ya Mashariki mti huu hupatikana kutoka pwani mpaka Ziwa Viktoria na karibu na Kigoma, Wilaya ya Uvinza.
Matunda haya yana ganda gumu lenye rangi ya kahawia hadi zambarau. Ladha yake ni uchachuuchachu pamoja na kuwa na sukari ndani yake. Tunda lina kiwango kikubwa cha vitamini C.
Hayalimwi lakini mara nyingi miti yake inatunzwa wakati wa kusafisha shamba. Pia matunda yake yanauzwa sokoni, kwa mfano Tabora mjini.
Tunda huliwa bichi au baada ya kulipika. Kwa kuipika shira tamu inapatikana.
Mizizi na matunda hupikwa na maji yake hutumika kama dawa ya asili na kutengenezea kinywaji. Matumizi ni kama tiba ya kisukari na kujisikia kizunguzungu.
Majina kwa lugha za kikabila
hariri- Kibena: sasati
- Kifipa: chinka, fulu
- Kihehe: fudululenga, sasati
- Kinyamwezi: sungwe
- Kinyaturu: sasati
- Kirangi: jumbau
- Kisukuma: gukubi, sungwi
- Kizigula: gobe
- Kizinza: kakata, sungwa
- Kiha: shindwi
- Kirundi: shindwi
Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Fundumaji kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |