Tabora (mji)

Tabora ni mji wa kihistoria ya Tanzania ya kati na makao makuu ya mkoa wa Tabora wenye postikodi namba 45100 [1]. Eneo lake ni manisipaa yenye hadhi ya wilaya. Mwaka 2012 palikuwa na wakazi 226,999.

Mazingira ya Tabora wakati wa mchana katika karne ya 19.
Tabora

Lua error in Module:Location_map at line 510: Unable to find the specified location map definition: "Module:Location map/data/Tanzania" does not exist.Mahali pa mji wa Tabora katika Tanzania

Majiranukta: 5°0′36″S 32°49′12″E / 5.01°S 32.82°E / -5.01; 32.82
Nchi Tanzania
Mkoa Tabora
Wilaya Tabora
Idadi ya wakazi
 - 188,808

HistoriaEdit

Mji ulianzishwa na wafanyabiashara Waarabu na Waswahili kutoka Zanzibar. Waliitumia kama kituo kwenye njia ya biashara ya misafara kati ya pwani na Ziwa Tanganyika katika nusu ya kwanza ya karne ya 19. Biashara kuu ilikuwa ndovu pamoja na watumwa. Tabora walijenga nyumba imara pamoja na ghala za bidhaa kwa ajili ya biashara hii. Familia ya Tippu Tip ilikuwa kati ya wenye nyumba wa Tabora.

Mwaka 1871 jeshi la rugaruga wa Mtemi Mirambo ilishambulia mji. Ukajengwa upya. Tangu 1890 Wajerumani walianza kufika na baada ya kushinda Wanyamwezi walifanya Tabora kuwa kitovu chao katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani ya kati; mji ukawa kituo cha kikosi cha jeshi na pia kikosi cha polisi.

Umuhimu wa Tabora ikaongezeka kwa ujenzi wa reli ya kati iliyounganisha pwani na Ziwa Tanganyika ikipita Tabora. Karahana muhimu ya reli ikawekwa hapa mjini. Wakati ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia pesa ya mwisho iliyotolewa na Wajerumani katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani ilitenengezwa katika karahana ya reli mwaka 1916 maana Dar es Salaam ilikuwa tayari mkononi mwa Waingereza.

1916 Tabora ilivamiwa na Wabelgiji waliowafukuza Wajerumani lakini baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia mji ukawa sehemu ya Tanganyika.

UsafiriEdit

Hadi leo Tabora ni kitovu muhimu cha mawasiliano cha Tanzania ya kati lakini barabara zote zinazofikia mji ni za udongo. Hata hivyo malori kutoka Daressalaam kuelekea Rwanda, Burundi au Kongo hupitia Tabora. Reli inapeleka abiria na mizigo kutoka Tabora kwenda Daressalaam, Kigoma na pia kwenda Mwanza kwa kutumia mkono wa kaskazini ya njia ya reli iliyojengwa wakati wa ukoloni wa Kiingereza.

Kuna pia uwanja mdogo wa ndege.

MarejeoEdit

  1. https://www.tcra.go.tz/images/documents/postcode/tabora.pdf[dead link]

Viungo vya njeEdit

  Kata za Manisipaa ya Tabora - Mkoa wa Tabora - Tanzania  

Chemchem | Cheyo | Gongoni | Ifucha | Ikomwa | Ipuli | Isevya | Itetemia | Itonjanda | Kabila | Kakola | Kalunde | Kanyenye | Kidongochekundu | Kiloleni | Kitete | Malolo (Tabora) | Mapambano | Mbugani | Misha | Mpela |Mtendeni | Mwinyi | Ndevelwa | Ng'ambo | Ntalikwa | Tambukareli | Tumbi | Uyui


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tabora bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Tabora (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.