GeoNames
GeoNames ni jina la hazinadata ya kijiografia kwenye intaneti. Hadi mwaka 2018 ilikuwa imekusanya tayari majina milioni 25 ya miji, vijiji, vitongoji, mikoa, milima, mito, misitu au maeneo mengine. Kati ya hizo ni sehemu milioni 4.8 zinazokaliwa na binadamu [1].
Data hizi zimekusanywa kutokana na zile zinazopatikana kutoka ofisi za serikali kote duniani lakini pia na hazinadata za taasisi nyingine kama BBC au Greenpeace. Zinapatikana katika intaneti kwa laiseni huria ya Creative Commons. Data hizo zinaweza kuwa na makosa kwa sababu haijawezekana bado kusanifisha hazinadata zote zilizotumiwa kama vyanzo.
Hata hivyo ni mkusanyo mkubwa wa data kati ya ile inayopatikana kwa umma kimataifa bila mashariti ya kibiashara[2].
Programu yake inatafuta jina na kuonyesha jina, nchi ambako jina hili linapatikana, "feature class" yaani ni aina gani ya mahali panapotajwa, na anwani ya kijiografia kwa umbo la majiranukta ya digrii, dakika na sekondi. Kutoka hapo ukurasa kwa kila mahali unafunguliwa ukionyesha pia majiranukta ya desimali halafu inawezekana kufungua ramani.
Marejeo
hariri- ↑ About GeoNames, tovuti ya wenyewe, iliangaliwa Juni 2019
- ↑ Majadiliano na muumbaji wa GeoNames, Mswisi Marc Wick Ilihifadhiwa 23 Julai 2021 kwenye Wayback Machine., tovuti ya goodgearguide.com 21 November, 2007, iliangaliwa Juni 2019
Viungo vya nje
hariri- https://www.geonames.org Tovuti ya GeoNames