"GETVALUE" ni shirika la biashara linalolenga faida lililo na makao makuu Dar es Salaam, nchini Tanzania, ambalo hutoa huduma za uuzaji na usambazaji wa bidhaa za kidijitali mtandaoni.

Nembo ya GETVALUE.

GETVALUE ni mmiliki wa tovuti iliyozinduliwa rasmi tarehe 15 Mei 2020 na Gaston Jackson Ngailo, aliyeanzisha shirika hilo mnamo tarehe 7 Disemba 2017.

Jina la GETVALUE linatokana na malengo ya Gaston Jackson Ngailo kuwa kila mtu atakayepata fursa ya kutumia GETVALUE basi apate thamani. Neno GETVALUE ni muunganiko wa maneno mawili ya lugha ya Kiingereza yaani neno “GET” likimaanisha “PATA” na neno “VALUE” likimaanisha “THAMANI”.Hivyo lengo ni muunganiko wa maneno hayo mawili kumaanisha "PATA THAMANI".[1]

GETVALUE
Taarifa Maelezo
Aina Ya Shirika Binafsi
Tasnia Biashara ya kielektroniki
Imezinduliwa 15 Mei, 2020
Ilianzishwa 7 Disemba, 2017
Muasisi Gaston Jackson Ngailo
Makao Makuu Dar es Salaam, Tanzania
Bidhaa/Huduma Vitabu,Vitabu Kwa Njia ya Sauti,

Mafunzo Kwa Njia ya Filamu,masoko shirikishi,

Nchi inayo hudumu Dunia nzima (Isipokuwa nchi ilipozuiliwa)
Mkurugenzi Mkuu Gaston Jackson Ngailo
Tovuti www.getvalue.co
Apilikesheni Ya Android Android
Apilikesheni Ya iOS iOS

Kwa sasa, GETVALUE imejikita zaidi katika kuuza vitabu. Kunapatikana aina mbalimbali za vitabu kuanzia vya ukufunzi wa maisha ,fedha , riwaya, dini, ualimu, ujenzi na ujasiriamali.

Kwa kutumia GETVALUE, unaweza kupata nakala laini ya kitabu mahali popote pale duniani. Pia mtandao unatoa huduma ya vitabu kwa njia ya sauti.

Viungo vya nje

hariri
  • [1] Tovuti rasmi
  • [2] programu-tumizi ya Android ya GETVALUE
  • [3] programu-tumizi ya iOS ya GETVALUE
  • [4] ukurasa wa Instagram wa GETVALUE
  • [5] ukurasa wa Facebook wa GETVALUE
  • [6] ukurasa wa Youtube wa GETVALUE
  • [7] ukurasa wa Twitter wa GETVALUE
  • [8] ukurasa wa Linkedin wa GETVALUE
  1. "Washindi Vodacom Digital Accelerator kutangazwa". Mwananchi (kwa Kiingereza). 2023-03-02. Iliwekwa mnamo 2023-03-08.
  Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu GetValue kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.