Gotardo wa Hildesheim

Gotardo wa Hildesheim, O.S.B. (jina asili: Gotthard au Godehard; Niederaltaich, Bavaria, 9604 Mei 1038) alikuwa mmonaki, padri, abati na hatimaye (2 Desemba 1022) askofu nchini Ujerumani[1].

Mt. Gotardo katika mavazi ya askofu, Hildesheim.

Kama kiongozi wa wamonaki, alitembelea na kuanzisha monasteri mbalimbali. Halafu kama askofu alijitahidi kustawisha jimbo lake, akirudisha nidhamu kati ya wakleri na kuunda shule kadhaa.

Papa Innocent II alimtangaza mtakatifu mwaka 1131.

Sikukuu yake huadhimishwa na Wakatoliki na Waorthodoksi tarehe 5 Mei[2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. www.santiebeati.it/dettaglio/51950
  2. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.