Tambarare kuu za Marekani
Tambarare kuu za Marekani (kwa Kiingereza: Great Plains) ni eneo kubwa la nchi hiyo lisilo na milima katika sehemu za kati na za magharibi za Marekani. Sehemu ya kaskazini inaingia ndani ya Kanada.
Upande wa magharibi zinaishia kwenye milima ya Rocky Mountains. Upande wa mashariki tambarare hizi zinapakana na maeneo ambako usimbishaji unaruhusu kustawi kwa misitu.
Majimbo yafuatayo ni sehemu za tambarare kuu:
- Maeneo yote ya Kansas, Nebraska, Dakota Kaskazini na Dakota Kusini (Marekani)
- Sehemu za Colorado, Montana, New Mexico, Oklahoma, Texas na Wyoming (Marekani)
- Sehemu za kusini za Alberta, Saskatchewan na Manitoba (Kanada)
Tabianchi huwa na miezi ya joto kali pamoja na miezi ya baridi sana. Uoto asilia wa nchi ulikuwa manyasi tu, maana mvua haitoshi kwa miti mingi.
Kabla ya kuja kwa Wazungu huko Marekani, tambarare kuu zilikuwa na ng'ombe mwitu aina ya baisoni kwa mamilioni waliowindwa na Maindio wahamaji na kuwa chakula chao kikuu.
Baisoni waliuawa kwa makusudi na Wamarekani weupe waliotaka kuondoa msingi wa kiuchumi wa Maindio na kutumia maeneo yao kwa kilimo. Sasa ni kitovu cha mazao ya nafaka kama mahindi na ngano ambazo hulisha mifugo na watu.
Tovuti za Nje
hariri- Chuo Kikuu cha Jimbo la Dakota Kaskazini: Hadithi ya Jiografia ya Tarafa Kubwa Ilihifadhiwa 5 Machi 2009 kwenye Wayback Machine.
- Kansas Heritage Group: Nyumba za Wenyeji, Uhifadhi, Maua, na Utafiti
- Maktaba ya Congress: Matawi mazuri
- Chuo Kikuu cha Nebraska-Lincoln: Utafiti Mkuu wa Matawi
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
|