Jangwa Kubwa la Victoria

(Elekezwa kutoka Great Victoria Desert)

Jangwa Kubwa la Victoria (Great Victoria Desert) ni jangwa kubwa zaidi nchini Australia. [1] Linaenea kwa km² 348,750 katika kusini magharibi ya bara hili. Uso wake ni mchanganyiko wa matuta ya mchanga, vilima vidogo, tambarare za nyasi, maeneo makubwa ya changarawe, na maziwa ya chumvi.

Jangwa kubwa la Victoria lililoonyeshwa kwa nyekundu.
Maralinga.

Jangwa hilo linapatikana katika majimbo ya Australia Magharibi na Australia Kusini. [2] Urefu wake kutoka mashariki hadi magharibi ni kama km 700.

Tabianchi ni yabisi sana, usimbishaji wa mwaka ni kati ya milimita 200 hadi 250 za mvua kila mwaka.

Lilipewa jina lake kwa heshima ya Malkia Viktoria wa Uingereza.

Wakazi asili wa Australia bado wanaishi katika sehemu ya jangwa wanapokalia eneo kubwa la kujitawala.

Marejeo

hariri
  1. Great Victoria Desert – The Largest Desert in Australia. Birgit Bradtke. Retrieved 26 March 2013.
  2. "Friends of the Great Victoria Desert - Facts and Figures". communitywebs.org. 2012 [last update]. Iliwekwa mnamo 1 November 2012. {{cite web}}: Check date values in: |year= (help)

Viungo vya Nje

hariri
  Makala hii kuhusu maeneo ya Australia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Jangwa Kubwa la Victoria kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.