Historia ya Omani
Historia ya Omani inahusu eneo ambalo leo linaunda Usultani wa Omani.
Hadi karne ya 18
haririOmani imekaliwa na watu kwa zaidi ya miaka 100,000.
Omani ilikuwa kituo muhimu cha biashara kwenye Bahari Hindi na Ghuba ya Uajemi tangu milenia mbili KK.
Tangu kuja kwa Uislamu Omani ilikuwa ama chini ya Uajemi au chini ya khalifa wa Baghdad na baadaye Dola la Seljuki.
Kati ya miaka 1507 na 1650 mji wa Maskat na pwani ya Omani vilitawaliwa na Ureno.
Makabila ya bara yaliunganika chini ya maimamu wa madhehebu ya Kiislamu ya Waibadiya na Imam Nasir ibn Murshid († 1649) alifaulu kupunguza eneo la Wareno. Mfuasi wake Sultan ibn Saif aliwafukuzwa kabisa Wareno na kushambulia vituo vyao kwenye pwani ya Afrika ya Mashariki.
Omani na Afrika ya Mashariki
haririMasultani wa Omani walitawala pwani ya Afrika ya Mashariki katika karne ya 19[1]. Mwaka 1830 Sultani Sayyid Said alihamisha mji mkuu wake kutoka Omani kuja mji wa Zanzibar (Unguja). Baada ya kifo chake mwaka 1856 dola liligawiwa kuwa nchi mbili:
- Usultani wa Omani
- Usultani wa Zanzibar
Maskat na Omani
haririTangu mwaka 1891 sultani alikuwa kabisa chini ya mamlaka ya mwakilishi Mwingereza hata kama kwa jina nchi haikuwa koloni. Kati ya makabila ya Omani bara ulikua upinzani dhidi ya utawala wa Sultani mjini Maskat na athira kubwa ya Uingereza katika serikali yake. Hali halisi kanda ya pwani ilikuwa chini ya sultani wa Maskat lakini katika sehemu za ndani, yaani Oman yenyewe, makabila yalijitawala au kuungana kumchagua imamu kama mkuu wao wa pamoja. Kwenye mwezi wa Mei mwaka 1913 viongozi wa makabila ya ndani pamoja na vongozi wa dini walikutana wakamchagua tena imamu.
Baada ya vita ya miaka 7 pande mbili zilipatana mwaka 1920 kugawa nchi: upande wa imamu ulikubali kutoshambulia tena miji ya vijiji vya pwani, sultani alikubali kuheshimu hali ya kujitawala ya maeneo ya ndani chini ya imamu[2]. Sehemu za ndani ziliendelea kujitawala chini ya imamu hadi mwaka 1954.
Muungano chini ya Sultani Taimur
haririAmani ilivunjwa mwaka 1954 wakati Sultani Said bin Taimur alitoa kibali kwa kampuni ya Kiingereza kutafuta mafuta ya petroli katika maeneo ya imamu. Kuingia kwa kikosi cha sultani kilichoongozwa na maafisa Waingereza kulikuwa chanzo cha vita iliyoendelea kwa miaka 5 hadi ushindi wa upande wa sultani aliyepata usaidizi wa jeshi la Uingereza. Hivyo Maskat na Omani iliunganishwa kwa nguvu ya kijeshi.
Sultani Said bin Taimur alipeleka mji mkuu wake kwenda Salalah akaendelea kutawala kutoka pale. Said bin Taimur alianza utawala wake akirithi madeni makubwa akalenga kumaliza deni na kutoingia madeni mapya. Hivyo alikataa uwekezaji katika miundombinu kama vile barabara au taasisi za elimu na afya. Hadi mwaka 1970 Omani ilikuwa na kilomita tu 10 za barabara za lami, hospitali 1 pekee na shule 3. Matumizi ya baisikeli na miwani ya Jua yalikatazwa na hapakuwa na simu kwa raia binafsi. Mageti ya miji iliyozungukwa bado na kuta zilifungwa wakati wa machweo. Wakati wa usiku kila raia alitakiwa kutembea akishika koroboi. Sultani mwenyewe aliangalia maombi yote ya viza kwa wageni waliotaka kuingia nchini, na vilevile vibali kwa wananchi waliotaka kutoka nje ya nchi.
Mapinduzi ya Qabus
haririKuanzia mwaka 1965 kulitokea uasi katika jimbo la Dhofar uliopanuka kati ya makabila ya milimani ukiongozwa na wanamapinduzi Wakomunisti kutoka nchi jirani ya Yemen Kusini. Jeshi la sultani lililoongozwa na maafisa Waingereza lilipambana na uasi huu na Waingereza walielewa kwamba sultani Taimur hakuwa na siasa ya kukomesha uasi. Hapo waliandaa mapinduzi ya kijeshi baada ya kuwasiliana na Qaboos bin Said al Said mwana pekee wa Taimur aliyewahi kusoma Uingereza lakini baada ya kurudi aliwekwa na baba yake chini ya ulinzi ndani ya kasri ya kifalme. Tarehe 23 Julai 1970 wanajeshi chini ya Waingereza walimkamata sultani Taimur aliyepelekwa mara moja uhamishoni Uingereza, Qabus alitangazwa kuwa sultani mpya.
Mabadiliko chini ya Qabus
haririTangu 1970 hadi 2019 Omani ilitawaliwa na sultani Qabus[3] aliyeanzisha mara moja mabadiliko mengi ya kufanya Omani kuwa nchi ya kisasa. Utumwa ulifutwa na mapato ya serikali, pamoja na hazina ya sultani, vilitumiwa kuwekeza katika miundombinu, ujenzi wa barabara, shule na hospitali. Vijana walitumwa ng'ambo ili wasome elimu ya kisasa.
Tangu miaka ya 1980, uwekezaji umelenga zaidi upande wa kuanzisha viwanda na kuanzisha kilimo cha kisasa ilhali nchi iliendelea kutegemea mapato ya uuzaji wa mafuta. Katika miaka 50 ya utawala wake nchi ilisogea mbele na mapato ya wananchi yaliongezeka mara 50.
Tanbihi
hariri- ↑ Benjamin Plackett (30 Machi 2017). Omani Music Masks A Slave Trading Past. Al-Fanar Media.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Jeremy Jones, Nicholas Ridout: A History of Modern Oman, uk. 91, Cambridge University Press, 2015 (google books)
- ↑ "Sultan Qaboos of Oman dies aged 79", BBC News, 11 January 2020. Retrieved on 10 January 2020.
Viungo vya nje
haririJua habari zaidi kuhusu Oman kwa kutafuta kupitia mradi wa Wikipedia Sister | |
---|---|
Uchambuzi wa kamusi kutoka Wikamusi | |
Vitabu kutoka Wikitabu | |
Dondoo kutoka Wikidondoa | |
Matini za vyanzo kutoka Wikichanzo | |
Picha na media kutoka Commons | |
Habari kutoka Wikihabari | |
Vyanzo vya elimu kutoka Wikichuo |
- Timeline of the Oman History from ancient civilization to modern day
- Chronology
- Omani Ministry of Foreign Affairs Ilihifadhiwa 7 Februari 2006 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Omani kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |