Historia ya Zambia
Historia ya Zambia inahusu eneo la Kusini mwa Afrika ambalo wakazi wake leo wanaunda Jamhuri ya Zambia.
Wakazi wa kwanza huaminiwa kuwa wawindaji wa jamii ya Wasani.
Katika karne za kwanza za milenia ya 1 BK walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi.
Baada ya wapelelezi Wazungu kufika katika karne ya 18, Zambia ikawa nchi lindwa ya Uingereza kwa jina la Northern Rhodesia mwishoni mwa karne ya 19.
Tarehe 24 Oktoba 1964, Zambia ikawa huru na waziri mkuu Kenneth Kaunda akawa rais wa kwanza.
Chama chake cha kijamaa United National Independence Party (UNIP) kilitawala kuanzia mwaka 1964 hadi 1991, kikiwa chama pekee halali kuanzia mwaka 1972.
Baada ya Kaunda kuanguka, Frederick Chiluba wa Movement for Multi-Party Democracy alitawala tangu mwaka 1991, akafuatwa na Levy Mwanawasa (2002-2008).
Aliyefuata tena ni rais Rupiah Banda (2008-2011), halafu Michael Sata wa Patriotic Front party (2008-2014).
Baada ya kifo chake, Guy Scott alikaimu hadi uchaguzi wa tarehe 20 Januari 2015, ambapo Edgar Lungu alipata kuwa rais wa sita.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Zambia kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |