Ibrahim Ajibu Migomba

mchezaji wa mpira wa miguu

Ibrahim Ajibu Migomba, (alizaliwa katika mkoa wa Singida tarehe 12 Septemba 1996) ni mchezaji wa mpira wa miguu nchini Tanzania. Anayecheza kama kiungo mshambuliaji katika klabu ya Coastal union ya Tanga inayoshiriki ligi kuu nchini Tanzania.

Ajibu akiwa katika mechi ya Simba Sports Club.

Ni mmoja kati ya wachezaji waliojaliwa kipaji cha hali ya juu na anatajwa kati ya wachezaji bora kuwahi kutokea Tanzania.

Ibrahim Ajibu ni kati ya wachezaji wachache Tanzania kuwahi kutoa pasi za kufunga (Assists) zaidi ya kumi kwa miaka minne mfululizo.

Uwanjani anatumia zaidi mguu wa kulia ingawa anaweza pia kucheza kama winga wa kushoto lakini kiasili Ajibu ni kiungo mshambuliaji.

Ajibu alijiunga kwenye accademy ya klabu ya Simba mwaka 2009,akiwa na umri wa miaka 13 na aliichezea Simba under-20 kabla ya kupandishwa kwenye timu ya wakubwa mwaka 2013 akiwa na miaka 17.

Aliishi Simba kwa misimu 4 na kuondoka akaenda kujiunga na club ya Yanga Sc kwa mkataba wa miaka 2 kwa dau zaidi ya Tsh 80,000,000 ambapo alicheza Yanga Sc hadi katikati ya mwaka 2019. Ajibu alikua ni nahodha wa Yanga na kupewa jezi maarufu ya nambari 10 kama heshima ya kipaji chake na kujitolea kwake katika klabu ya Yanga Huko Yanga katika mechi 55 alifunga magoli 46.

Ajibu ni mtaalamu wa pasi za mwisho (assist) ambapo katika ligi ya Tanzania 2018/19 ameweza kutengeneza magoli kumi na tisa, akifunga 6 yeye mwenyewe

Hadi sasa goli la Ajibu dhidi ya Mbao Fc linazungumziwa kuwa ni goli bora kuwahi kufungwa Tanzania.

Ibrahim Ajib, baada ya kumaliza mkataba wake katika klabu ya Yanga alijiunga na klabu ya Simba sc kwa mkataba wa miaka miwili huku akilipwa zaidi ya Tsh 100,000,000 pamoja na kupewa gari la fahari.

Anajulikana pia kuwa mchezaji mwenye utajiri mkubwa wa mali na fedha kwa wanaocheza katika ligi kuu ya Tanzania. Ajibu hapendi kuweka maisha yake binafsi kwenye jamii, ila inasemekana kuwa ana nyumba zipatazo 4 za fahari kwenye jiji la Dar es Salaam, magari ya kutembelea tofauti, biashara binafsi pamoja na mashamba makubwa nchini Tanzania. Ajibu ni mchezaji anayependwa sana na Watanzania kwani kuna nyimbo nyingi wasanii humpa sifa lukuki kwa kipaji chake maridhawa cha mpira.

Ibrahim Ajibu ndiye mchezaji namba moja kwa mvuto wa kibiashara nchini Tanzania kwani ndiye mchezaji anayeongoza kwa matangazo ya kampuni tofauti kama vile Serengeti Breweries, King'amuzi cha StarTimes, Kanzu Point na nyinginezo.

Ajibu yupo chini ya kampuni ya uwakala inayoitwa Kessy Marketing Agency iliyopo Dar es Salaam, Tanzania. Hata hivyo kuna msimu alipelekwa kwa mkopo timu ya Mwadui Fc iliyopo mkoani shinyanga kwaajili ya kukuza kipaji chake.

Ibrahim Ajibu ni muumini wa dini ya Kiislamu, ana mke na watoto 2, mmoja wa kike na mmoja wa kiume. Pia ni mtaalamu wa kuogelea.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ibrahim Ajibu Migomba kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.