Ignas wa Antiokia
Ignas wa Antiokia (kwa Kigiriki Ἰγνάτιος, Ignatios; alijulikana pia kwa jina la Θεοφόρος, Theophoros, yaani "Mleta Mungu"; 35/50 B.K. - 98/117[1]).
Ni kati ya Mababu wa Kanisa wa kwanza, akiwa mwanafunzi wa Mtume Yohane na askofu wa tatu wa Antiokia, leo nchini Uturuki.
Chini ya kaisari Traiano, alihukumiwa kuliwa na wanyamapori, na kwa ajili hiyo alifikishwa Roma alipofia dini yake: safarini, huku akionja ukatili wa walinzi wake, alioufananisha na ule wa chui, aliandika barua kwa makanisa mbalimbali na kwa Polikarp Mtakatifu , alimohimiza ndugu zake katika imani kumtumikia Mungu katika ushirika na maaskofu na wasimzuie kuchinjwa sadaka kwa Kristo[2].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake inaadhimishwa na Wakatoliki[3][4], Waanglikana na Waorthodoksi wa Mashariki kwenye 17 Oktoba, lakini na Waorthodoksi tarehe 20 Desemba.
Maandishi yake
haririKati ya barua zake, zimetufikia saba za hakika ambazo ni kama kielelezo cha teolojia ya awali ya Ukristo. Humo kwa mara ya kwanza tunasoma juu ya Kanisa Katoliki ambalo linaitwa hivi kwa kulitofautisha na makundi ya Wakristo waliotengana nalo.
Kati ya mada muhimu zaidi kuna Kanisa, sakramenti na nafasi ya askofu pekee katika kila jimbo.
Barua zake zimetafsiriwa kwa Kiswahili na kutolewa Italia kama ifuatavyo: MT. IGNASI WA ANTIOKIA, Nyaraka - tafsiri ya B. Santopadre n.k. – ed. E.M.I. – Bologna 1992 – ISBN 88-307-0404-0
Tazama pia
haririMarejeo
hariri- ↑ Tazama: "Ignatius" katika The Westminster Dictionary of Church History, ed. Jerald Brauer (Philadelphia:Westminster, 1971) na pia David Hugh Farmer, "Ignatius of Antioch" katika The Oxford Dictionary of the Saints (New York: Oxford University Press, 1987).
- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/24900
- ↑ Calendarium Romanum (Vatican City, 1969)
- ↑ Martyrologium Romanum
Viungo vya nje
hariri- http://web.archive.org/web/20080121044055/http://www.earlychristianwritings.com/ignatius.htmlEarlyChristianwritings: On-line texts of St. Ignatius' letters (archived)] (non-archived linkIlihifadhiwa 21 Januari 2008 kwenye Wayback Machine.)
- Catholic Encyclopedia: St. Ignatius of Antioch
- The Short Syriac Version Ilihifadhiwa 18 Machi 2009 kwenye Wayback Machine.
- The Ecclesiology of St. Ignatius of Antioch by Fr. John S. Romanides
- Saint Ignatius Ilihifadhiwa 30 Agosti 2009 kwenye Wayback Machine.
- Opera Omnia by Migne Patrologia Graeca with analytical indexes
- Catholic Encyclopedia: Spurious Epistles of St. Ignatius of Antioch
- Holy Letters and Syllables, the function and character of Scripture Authority in the writings of St Ignatius (Contains biography Ignatius as well. Doctoral thesis University of the Orange Free State 1997, Dutch, pdf) Ilihifadhiwa 22 Septemba 2009 kwenye Wayback Machine.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |