Ignas wa Antiokia
Ignas wa Antiokia (kwa Kigiriki Ἰγνάτιος, Ignatios: lakini alijulikana pia kwa jina la Θεοφόρος, Theophoros, yaani "Mleta Mungu") alizaliwa kati ya miaka 35 na 50 B.K. akafa kati ya 98 na 117.[1]

Ni kati ya Mababu wa Kanisa wa kwanza, akiwa askofu wa tatu wa Antiokia na mwanafunzi wa Mitume wa Yesu.
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake inaadhimishwa na Waorthodoksi tarehe 20 Desemba, lakini na Wakatoliki, Waanglikana na Waorthodoksi wa Mashariki kwenye 17 Oktoba.[2]
Maandishi yakeEdit
Akielekea kifodini chake huko Roma, aliandika barua kadhaa kwa makanisa na kwa Polikarp Mtakatifu ambazo 7 za hakika zimetunzwa kama kielelezo cha teolojia ya awali ya Ukristo. Humo kwa mara ya kwanza tunasoma juu ya Kanisa Katoliki ambalo linaitwa hivi kwa kulitofautisha na makundi ya Wakristo waliotengana nalo.
Kati ya mada muhimu zaidi kuna Kanisa, sakramenti na nafasi ya askofu pekee katika kila jimbo.
Barua zake zimetafsiriwa kwa Kiswahili na kutolewa Italia kama ifuatavyo: MT. IGNASI WA ANTIOKIA, Nyaraka - tafsiri ya B. Santopadre n.k. – ed. E.M.I. – Bologna 1992 – ISBN 88-307-0404-0
Tazama piaEdit
MarejeoEdit
- ↑ Tazama: "Ignatius" katika The Westminster Dictionary of Church History, ed. Jerald Brauer (Philadelphia:Westminster, 1971) na pia David Hugh Farmer, "Ignatius of Antioch" katika The Oxford Dictionary of the Saints (New York: Oxford University Press, 1987).
- ↑ Calendarium Romanum (Vatican City, 1969).
Viungo vya njeEdit
- http://web.archive.org/web/20080121044055/http://www.earlychristianwritings.com/ignatius.htmlEarly Christian writings: On-line texts of St. Ignatius' letters (archived)] (non-archived linkArchived Januari 21, 2008 at the Wayback Machine.)
- Catholic Encyclopedia: St. Ignatius of Antioch
- The Short Syriac Version
- The Ecclesiology of St. Ignatius of Antioch by Fr. John S. Romanides
- Saint Ignatius
- Opera Omnia by Migne Patrologia Graeca with analytical indexes
- Catholic Encyclopedia: Spurious Epistles of St. Ignatius of Antioch
- Holy Letters and Syllables, the function and character of Scripture Authority in the writings of St Ignatius (Contains biography Ignatius as well. Doctoral thesis University of the Orange Free State 1997, Dutch, pdf) Archived Septemba 22, 2009 at the Wayback Machine.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |