Ignas wa Antiokia

(Elekezwa kutoka Ignatius of Antioch)

Ignas wa Antiokia (kwa Kigiriki Ἰγνάτιος, Ignatios; alijulikana pia kwa jina la Θεοφόρος, Theophoros, yaani "Mleta Mungu"; 35/50 B.K. - 98/117[1]).

Kifodini cha Mt. Ignas.

Ni kati ya Mababu wa Kanisa wa kwanza, akiwa mwanafunzi wa Mtume Yohane na askofu wa tatu wa Antiokia, leo nchini Uturuki.

Chini ya kaisari Traiano, alihukumiwa kuliwa na wanyamapori, na kwa ajili hiyo alifikishwa Roma alipofia dini yake: safarini, huku akionja ukatili wa walinzi wake, alioufananisha na ule wa chui, aliandika barua kwa makanisa mbalimbali na kwa Polikarp Mtakatifu , alimohimiza ndugu zake katika imani kumtumikia Mungu katika ushirika na maaskofu na wasimzuie kuchinjwa sadaka kwa Kristo[2].

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake inaadhimishwa na Wakatoliki[3][4], Waanglikana na Waorthodoksi wa Mashariki kwenye 17 Oktoba, lakini na Waorthodoksi tarehe 20 Desemba.

Maandishi yake

hariri

Kati ya barua zake, zimetufikia saba za hakika ambazo ni kama kielelezo cha teolojia ya awali ya Ukristo. Humo kwa mara ya kwanza tunasoma juu ya Kanisa Katoliki ambalo linaitwa hivi kwa kulitofautisha na makundi ya Wakristo waliotengana nalo.

Kati ya mada muhimu zaidi kuna Kanisa, sakramenti na nafasi ya askofu pekee katika kila jimbo.

Barua zake zimetafsiriwa kwa Kiswahili na kutolewa Italia kama ifuatavyo: MT. IGNASI WA ANTIOKIA, Nyaraka - tafsiri ya B. Santopadre n.k. – ed. E.M.I. – Bologna 1992 – ISBN 88-307-0404-0

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri
  1. Tazama: "Ignatius" katika The Westminster Dictionary of Church History, ed. Jerald Brauer (Philadelphia:Westminster, 1971) na pia David Hugh Farmer, "Ignatius of Antioch" katika The Oxford Dictionary of the Saints (New York: Oxford University Press, 1987).
  2. https://www.santiebeati.it/dettaglio/24900
  3. Calendarium Romanum (Vatican City, 1969)
  4. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.