Joanisi (pia: Joanisi Mkuu, kwa Kigiriki: Όσιος Ιωαννίκιος ο Μέγας; Bitinia, 754/762 hivi - Antidium, 3 Novemba 846) alikuwa mmonaki, na hasa mkaapweke, maarufu kwa miujiza[1], katika maeneo ya Uturuki ya leo. Alisaidia kurudisha heshima kwa picha takatifu baada ya dhuluma ya serikali ya Dola la Roma Mashariki[2].

Picha takatifu ya Mt. Joanisi Mkuu.
Mji wa Bursa kutoka Mlima Uludag, alipoishi miaka mingi na unaoitwa hadi leo "Mlima wa Wamonaki".

Kabla ya kutawa alikuwa askari kwa miaka 20[3][4]. Baada ya hapo alijitoa kuishi upwekeni kwenye miteremko ya mlima, akimalizia kwa kawaida sala na maneno haya: «Ee Mungu, tumaini langu; ee Kristo, kimbilio langu; ee Roho Mtakatifu, msimamizi wangu»[5].

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila tarehe 3 Novemba[6] au 4 Novemba [7][8].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. Butler, Rev. Alban (2010). The Lives of the Saints. New York: Bartelby.
  2. "Venerable Joannicius the Great". Orthodox Church In America. Iliwekwa mnamo Julai 3, 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Treadgold, Warren (Januari 2002). "Photius Before His Patriarchate". Journal of Ecclesiastical History. 53 – kutoka Cambridge.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Cyril Mango, "The Two Lives of St Ioannikios and the Bulgarians", Harvard Ukrainian Studies VII (1983) (Okeanos: Essays presented to Ihor Swevcenko),393-404, esp. pp.396-400
  5. http://www.santiebeati.it/nomi/Detailed/76060.html
  6. Martyrologium Romanum
  7. Συναξαριστής. 4 Νοεμβρίου. ECCLESIA.GR. (H ΕΚΚΛΗΣΙΑ ΤΗΣ ΕΛΛΑΔΟΣ).
  8. Ὁ Ὅσιος Ἰωαννίκιος ὁ Μέγας ὁ ἐν Ὀλύμπῳ. 4 Νοεμβρίου. ΜΕΓΑΣ ΣΥΝΑΞΑΡΙΣΤΗΣ.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.