John William Kijazi

John William Kijazi (18 Novemba 1956 [1] - 17 Februari 2021[2] [3]) hadi kifo chake alikuwa katibu mkuu kiongozi katika utawala wa rais John Pombe Magufuli.

Alisoma uhandisi kwenye vyuo vikuu vya Dar es Salaam na Birmingham miaka 1982 - 1992 akaajiriwa na Wizara ya Ujenzi ya Tanzania na kupanda ngazi hadi kuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo.

Mwaka 2007 alihamia Wizara ya Mambo ya Nje akawa balozi wa Tanzania nchini Uhindi.

Mwaka 2016 aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu kiongozi katika serikali ya rais Magufuli.

Marejeo

hariri
  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-01-31. Iliwekwa mnamo 2021-02-19.
  2. https://www.mwananchi.co.tz/mw/habari/kitaifa/balozi-kijazi-afariki-dunia-3295348
  3. https://citizentv.co.ke/news/another-top-tanzanian-govt-official-john-william-kijazi-dies-6632424/
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu John William Kijazi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.