Joji, Aureli na wenzao

Joji, Aureli na wenzao Natalia (jina la awali: Sabigoto), Felisi na Liliosa (walifariki Cordoba, leo nchini Hispania, 852) walikuwa Wakristo waliokatwa kichwa chini ya utawala wa Waislamu.

Joji alikuwa shemasi mmonaki kutoka Syria-Palestina. Wenzake walikuwa watu wa ndoa wenyeji[1].

Wakitamani kushuhudia imani yao kwa kufia dini, walipotupwa gerezani hawakuacha kumuimbia sifa Kristo.

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 27 Julai [2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.